Brainfood

76 Pins
 16w
Collection by
HOW TO LEARN FASTER | LAW OF ATTRACTION THINGS #attractionoflaw #lawattraction #lawofattractionlifecoaching #lawofattractionbook #lawofattractionbabe #lawofattractionplannerw Study Skills, Skills To Learn, Life Skills, Life Lessons, Personal Development Skills, Self Development Books, Life Improvement
Way2Manifest
HOW TO LEARN FASTER | LAW OF ATTRACTION THINGS #attractionoflaw #lawattraction #lawofattractionlifecoaching #lawofattractionbook #lawofattractionbabe #lawofattractionplannerw
Infographic: 7 YouTubers to Help You Learn While Sleeping | SleepPhones® Comfortable Headband Headphones for Sleeping College Life Hacks, Life Hacks For School, School Study Tips, College Study, Learning Languages Tips, Foreign Languages, Student Hacks, E Mc2, Useful Life Hacks
Infographic: 7 YouTubers to Help You Learn While Sleeping
Infographic: 7 YouTubers to Help You Learn While Sleeping | SleepPhones® Comfortable Headband Headphones for Sleeping
Research Skills, Research Methods, Writing Skills, Student Life Hacks, Study Tips College
Learn How to Research Any Topic - Public Generalist
Public Generalist | Self-Improvement And Educational Blogger
Public Generalist | Self-Improvement And Educational Blogger
Studio Equipment, Album Songs, Best Songs, Rappers, Spotify, Podcasts, Episode
Jasusi - Jinsi ya Kuwa Mtu Bora S01E03: Tabia 14 Zinavyokwamisha Maendeleo ya Mtu
Healthy Food Swaps, Healthy Foods To Eat, Health Healthy, Health And Nutrition, Healthy Tips, Healthy Habits, Health And Wellness, Healthy Drinks, Healthy Body
Turmeric Water Uses - Organic Advices
Norma LindemannN
Norma Lindemann
#WordOfTheDay
Evarist Chahali
Evarist Chahali
#WordOfTheDay
Evarist Chahali
Evarist Chahali
Related searches
Evarist Chahali on Instagram: “Heri ya Siku ya Wapendanao. Moja ya matamanio ya wapendanao ni kuwa na mwenza aliye bora. Na katika kuadhimisha siku hii, ninakuorodheshea…” Instagram
Evarist Chahali on Instagram: “Heri ya Siku ya Wapendanao. Moja ya matamanio ya wapendanao ni kuwa na mwenza aliye bora. Na katika kuadhimisha siku hii, ninakuorodheshea…”
The 99 best things that happened in 2017 – Evarist Chahali – Medium Good Things, Shit Happens, Medium, Best, Medium Long Hairstyles
The 99 best things that happened in 2017
The 99 best things that happened in 2017 – Evarist Chahali – Medium
Nimeandika kwa kirefu katika kitabu changu kipya cha kielektroniki “Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota… John Magufuli, Edwin, Safari, Baseball Cards, Sports, Hs Sports, Sport
Wanasiasa CCM vs Maaskofu, Mashehe vs Maaskofu: Chonde Chonde Magufuli
Nimeandika kwa kirefu katika kitabu changu kipya cha kielektroniki “Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota…
100+ Google Tricks. Many great tips I would have never known about without this pin Teacher Tech, Teacher Tools, Teacher Hacks, Teacher Resources, Teaching Ideas, Teaching Technology, School Technology, Technology Integration, Technology Tools
Google for Teachers: 100+ Tricks
100+ Google Tricks. Many great tips I would have never known about without this pin
Uchambuzi Wa Kina Kuhusu Nyalandu Kuhama CCM Na Kuomba Kujiunga Chadema  Pasipo kutarajiwa jana Jumatatu ya Oktoba 30 2017 anga za habari huko nyumbani Tanzania zilitawaliwa na habari moja nzito: mmoja wa wana-CCM maarufu Mbunge kwa tiketi ya chama hicho tawala anayewakilisha jimbo la Singida Kaskazini na Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Nne Bwana Lazaro Nyalandu alitangaza kujivua uanachama wa CCM na kuomba kujiunga na chama kikuu cha upinzani cha Chadema. Tukio hilo lilileta msh Lazaro, Libya, Tanzania, Hospitality, Global, Paper, Rhinos, Elephants, News
Uchambuzi Wa Kina Kuhusu Nyalandu Kuhama CCM Na Kuomba Kujiunga Chadema
Uchambuzi Wa Kina Kuhusu Nyalandu Kuhama CCM Na Kuomba Kujiunga Chadema Pasipo kutarajiwa jana Jumatatu ya Oktoba 30 2017 anga za habari huko nyumbani Tanzania zilitawaliwa na habari moja nzito: mmoja wa wana-CCM maarufu Mbunge kwa tiketi ya chama hicho tawala anayewakilisha jimbo la Singida Kaskazini na Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Nne Bwana Lazaro Nyalandu alitangaza kujivua uanachama wa CCM na kuomba kujiunga na chama kikuu cha upinzani cha Chadema. Tukio hilo lilileta msh
Uchambuzi Wa Kina: Nini Hasa Kimemfanya Magufuli Abadilike Kiasi Hiki?  Mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka juzi nilipata ujumbe kutoka kwa watu kadhaa wakinieleza kuwa kwa namna moja au nyingine niliwasaidia kufanya maamuzi ya kumpigia kura aliyekuwa mgombea wa CCM John Magufuli. Unajua moja ya makosa makubwa waliofanya wana-UKAWA kwenye kampeni za uchaguzi huo ni kutojihangaisha kulifikia kundi muhimu la wapigakura nchini Tanzania: wananchi wasiofungamana na chama chochote. Ili kulielewa vema kundi hili inabidi kuangalia idadi ya wanachama wa CCM na UKAWA (kwa kuzingatia uchaguzi wa mwaka 2015). Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa CCM ina wanachama milioni 8. Makadirio ya idadi ya wanachama wa UKAWA ni angalau milioni 5. Kwahiyo makadirio ya jumla ya wapigakura wenye kufungamana na vyama vya siasa ni takriban milioni 13. Tanzania ina watu zaidi ya milioni 50 tukitoa hao milioni 13 tunabakiwa na watu milioni 37. Tukienda kwenye idadi ya waliojiandikisha kupiga kura walikuwa milioni 23 hivi. Kwahiyo kimahesabu takriban watu milioni 10 (milioni 23 waliojiandikisha kutoa milioni 13 wenye ufuasi wa vyama vya siasa) walikuwa wapigakura wasiojihusisha na chama chochote. Tofauti na UKAWA ambayo viongozi na wanachama wake walielemea zaidi kuhamasishana wao kwa wao wenzao wa CCM waliwalenga hao takriban milioni 10 wasiofungamana na chama chochote.  Na kimsingi mie japo sikuwa mpigakura nilikuwa katika kundi la watu wasio na vyama. Mara ya mwisho kuwa mwanachama wa chama cha siasa ilikuwa mwaka 2005 na takriban miaka 15 baadae sheria ilinizuwia kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Mwaka 2006 nilianza kufuatilia skandali ya Richmond iliyokuwa ikimhusisha aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa. Naweza kwa uhakika kuwa nilikuwa bloga pekee niliyevalia njua suala hilo sambamba na kuliandikia makala mbalimbali katika magazeti ya Kulikoni na baadaye Mtanzania na hatimaye Raia Mwema. Ufuatiliaji huo ulinigharimu mno lakini hilo si la muhimu kwa sasa. Kutokana na bughudha niliyopata kuanzia mwaka 2006 na kuendelea haikuwa ajabu kwa mie kuunga mkono harakati za Chadema kupambana na ufisadi. Na mwaka 2010 nilishiriki kikamilifu kumnadi mgombea urais wa Chadema Dkt Wilbrord Slaa. Hata baada ya uchaguzi huo niliendelea kuunga mkono sera hiyo ya ufisadi ya Chadema.Hata hivyo sikuwahi kuwa mwanachama wa chama hicho. Mwanzoni mwa mwaka 2015 nilikuwa miongoni mwa watu waliopiga kelele kwenye mitandao ya kijamii kuwataka UKAWA watangaze mgombea wao wa kiti cha urais mapema hasa ikizingatiwa kuwa CCM walikuwa na safari ndefu ya kungoana macho kugombea kuteuliwa na chama chao kuwania urais. Hata hivyo kelele hizo hazikuzaa matunda na utetezi mkubwa ulikuwa UKAWA inajibidiisha kushughulikia daftari la wapigakura sambamba na kuhamasisha wapigakura watarajiwa kujiandikisha. Hatimaye tulikuja kufahamu kuwa mbinu hiyo ya kununua muda ililenga kumwandalia nafasi Bwana Lowassa endapo asingepitishwa huko CCM. Muungano wa vyama makini vinne vya upinzani unasubiri kapi kutoka chama tawala! Kufupisha stori mara baada ya UKAWA kumtangaza Lowassa kuwa mgombea wao kwa sie wengine ilikuwa haiwezekani tena kuunga mkono umoja huo uliojumuisha vyama vya Chadema CUF NCCR-Mageuzi na NLD.  Kwa vile wagombea wakuu katika uchaguzi huo walikuwa Lowassa na Magufuli ilikuwa vigumu kumpinga Lowassa bila kumsapoti Magufuli. Kwahiyo japo awali nilijaribu kuepuka kumnadi mgombea wa CCM Magufuli mazingira yaliyokuwepo pamoja na mkataba wa kutoa huduma ya usadi (consultancy) ilipelekea nami nianze kumnadi Magufuli. Haukuwa uamuzi rahisi hasa kwa kuzingatia serikali ya CCM ilivyonitenda kuanzia mwaka 2006 nilipoanza kufuatilia skandali ya Richmond.  Ushiriki wangu kwenye kampeni haukuwa rahisi. Katika maisha yangu yote sikuwahi kutukanwa kiasi nilichotukanwa katika kampeni za uchaguzi huo. Jitihada zangu za kuwaelewesha watu kwanini nimelazimika kumuunga mkono Magufuli hazikusaidia kitu. Pengine kibaya zaidi ni kwamba wakati wa kuelekea uchaguzi huo nilifiwa na baba yangu marehemu Mzee Philemon Chahali. Baadhi ya watu bila utu walitumia msiba huo kuingiza uhasama wa kisiasa.  Pamoja na mvua ya matusi ya kila aina niliendelea na jukumu la kumnadi Bwana Magufuli. Nadhani mchango wangu mkubwa zaidi ulikuwa kwa wapigakura waliokuwa hawajafungama na chama chochote. Na nilifahamu kuhusu hilo baada ya uchaguzi ambapo baadhi yao walinieleza bayana kuwa ushawishi wangu kwao ulipelekea kufanya uamuzi wa kumpigia kura mgombea huyo wa CCM. Lakini tukiweka kando sababu zangu binafsi Magufuli alionekana kama mgombea bora zaidi ya mpinzani wake Lowassa. Pamoja na sababu nyingine wakati Magufuli alikuwa mgombea wa CCM kutoka CCM Lowassa alikuwa mgombea wa UKAWA kutoka CCM.  Hatimaye uchaguzi ukafanyika na Magufuli akaibuka mshindi. Kama kuna kitu kilichonipa matumaini sana kuhusu urais wa Magufuli ni hotuba yake aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa bunge la Jamhuri ya Muungano. Katika hotuba hiyo Magufuli alionyesha kuwa mtu anayezielewa vema shida za Watanzania hususan janga la rushwa na ufisadi na akaapa kushughulikia kwa nguvu zake zote. Na alipoomba Watanzania wamwombee katika vita hiyo ngumu naamini hata miongoni mwa wale ambao hawakumpigia kura waliitikia wito huo wa kumfanyia maombi. Kisha zikaja ziara ya kushtukiza na taratibu tukaanza kuingiwa na matumaini mapya ya mrithi halisi wa Nyerere/Sokoine. Na dunia pia ikaungana nasi kusherehekea kiongozi huyo adimu na ikaibuka alama ya reli #WhatWouldMagufuli Do iliyotamba kila kona ya dunia. Na haikupita wiki bila kushuhudia tumbua majipu.  Kwa kufurahishwa na kuridhishwa na utendaji wake mie nikajipinda na kuandika kitabu cha tathmini ya urais wa Magufuli siku 55 tu baada ya yeye kuapishwa kuwa Rais wa tano wa Tanzania. Watu kadhaa walinikosoa kwamba haikuwa sahihi kwangu kufanya tathmini hiyo mapema kiasi hicho. Kwa wakati huo niliona walionikosoa kuhusu suala hilo kama watu wenye chuki binafsi dhidi ya mkombozi Magufuli.  Dalili ya kwanza kwamba huenda kuna walakini katika utawala wa Magufuli ni pale alipotangaza baraza lake la mawaziri ambalo ilituchukua wiki kadhaa kulisubiri. Lilipotangazwa sio tu lilikuwa kubwa kuliko ahadi yake kuwa angeunda serikali ndogo tu ili kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali bali pia lilijumuisha baadhi ya sura zenye utata. Miongoni mwa sura hizo ni Profesa Muhongo ambaye alilazimika kujiuzulu katika serikali ya Awamu ya Nne kutokana na kuhusishwa na skandali ya Tegeta Escrow.  Kuna tuliouona uteuzi wa mtu kama Nape Nnauye kuwa ni wa kisiasa zaidi huku sura kama Simbachawene Lukuvi na Profesa Maghembe zikijenga ishara kuwa huenda mambo hayajabadilika kama tulivyotarajia. Kisha kukafanyika uteuzi wa mabalozi ambao ulionekana bayana kama kutumia nafasi hizo nyeti kuwaondoa watu flani kwenye nyadhifa zao huko CCM. Baadhi yetu tukaanza kujiuliza hivi hatujayashuhudia haya huko nyuma? Lakini tukaendelea kuwa na matumaini. Dalili ya kwanza kabisa kuwa pamoja na mazuri yake yaliyowavutia Watanzania wengi na kona mbalimbali duniani Bwana Magufuli ana mapungufu yake ni pale serikali yake kupitia shujaa wa sasa Nape Nnauye ilipozuwia haki ya mamilioni ya Watanzania kusikiliza matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. Niwe mkweli wanaomwona Nape shujaa huwa siwaelewi kabisa. Ningemwona shujaa laiti angetumia ukongwe wake ndani ya CCM kumweleza bosi wake Magufuli kuwa wazo la kuzuwia matangazo ya bunge live ni fyongo na laiti Magufuli angemomea basi angejiuzulu kishujaa badala ya kusubiri kufukuzwauwaziri kwa kupambana na kimeo kingine cha Magufuli yaani Daudi Albert Bashite. Baadaye likaja zuwio dhidi ya mikutano na maandamano ya vyama ya siasa. Awali baadhi yetu tulijipa matumaini kwamba ah huu ni muda wa kuchapa kazi. Hayo maandamano na mikutano ni ya nini muda huu? Kwahiyo kwa wakati huo ili-make sense. Mara tukakumbwa na janga la tetemeko la ardhi huko Kagera. Ikategemewa Rais angekwenda kuwafariji wahanga hasa ikizingatiwa kuwa anatoka Kanda ya Ziwa. Hakwenda hadi baadaye. Na alipokwenda akatoa hotuba isiyopendeza kuisikiliza. Maneno kama serikali haikuleta tetemeko la ardhi sio ya busara hata kidogo. Pia akaongopa kwa kudai hakuna serikali duniani inayotoa misaada kwa wahanga wa majanga ya asili. Sijui muda huu anajisikiaje akiona kwenye runinga jinsi serikali ya Marekani inavyowahudumia wahanga wa vimbunga. Baadaye kukusikika taarifa mbalimbali za tishio la uhaba wa chakula lakini badala ya kuwafariji wananchi Magufuli akawaropokea kwamba serikali yake haitotoa chakula kwa vile serikali haina shamba.  Na wakati mmoja alipita sijui Nzega au Urambo mwananchi mmoja akamwambia njaa Mheshimiwa. Hilo jibu alilotoa utadhani ugomvi. Pamoja na majibu mengine ya ngebe akasema njaa kwani mnataka niingie jikoni kuwapikia? Ovyo kabisa. Likatokea tukio la maaskari polisi wanane kuuawa huko Kibiti lakini Amiri Jeshi Mkuu akaenda kufungua mabweni chuo kikuu cha Dar es Salaama badala ya kwenda kuaga miili ya askari hao. Pia kulijitokeza tukio la kupotea kwa kada wa Chadema Ben Saanane ambaye hadi kupotea kwake alikuwa akihoji kwa nguvu kubwa kuhusu PhD ya Magufuli. Baadhi tulimsihi awe makini (kwa sababu dalili zilishaanza kujionyesha kuwa Magufuli ni mtu wa aina gani) lakini bahati mbaya hakusikia ushauri wetu. Hadi leo haijulikani nini kimemsibu kijana huyo japo Chadema nao hawawezi kukwepa lawama katika poor handling ya suala hilo. Kumekuwa na kauli zinazokinzana kutoka kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho kama ile ya mwenyekiti Mbowe kuwa Ben alitekwa huku Mbunge wa chama hicho Saeid Kubenea akidai kuwa kada huyo anaonekana vijiweni. Kwanini chama hicho hakijawabana viongozi hao kufafanua kauli zao only God knows! Lakini kama kuna tukio lililompotezea heshima kubwa Bwana Magufuli ni lile la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kuvamia stesheni ya redio na runinga cha Clouds akiwa na askari wenye silaha. Siku chache baadaye huku baadhi ya watu wakitarajia angemtimua Makonda Magufuli akatufanya sote mabwege kwa kumtetea Makonda huku akidai yeye hapangiwi kazi yeye ndo Rais na kumwita Makonda mchapakazi. Yaani Mkuu wa Mkoa amevamia kituo cha habari kitendo ambacho ni kosa la jinai halafu Rais anamsifu kuwa ni mchapakazi?  Uswahiba wa Magufuli na Makonda umechangia mno ugumu wa kuchunguza tuhuma kuwa mkuu huyo wa mkoa amefoji jina analotumia pamoja na cheti cha kuhitimu kidato cha nne. Laiti Magufuli angekuwa mwajibikaji kama tunavyoamini basi angeamuru uchunguzi kuhusu suala hilo.  Na kwa wanaofahamu yanayoendelea nyuma ya pazia inadaiwa kuwa vetting aliyofanyiwa Bashite ilionyesha bayana mapungufu yanatajwa kumhusu yeye na Bwana mkubwa akashauriwa kuchukua hatua stahili lakini hakufuata ushauri huo. Hili la Bashite limeendelea kuwakera watu wengi sana hasa ikizingatiwa kuwa mtu huyo anatumia ipasavyo upendeleo anaopewa na Magufuli na kufanya dharau za wazi kama ile ya kupigiwa saluti na vingozi wa ngazi za juu wa jeshi la polisi huku amevaa kapelo. Hiyo ni dharau ya hali ya juu kwa vyombo vyetu vya dola. Na Magufuli ataingia kwenye vitabu vya historia kwa serikali yake kulifungia gazeti la kila wiki la Mwanahalisi kwa miaka mitatu na siku 10 baadaye akalifungia gazeti jingine la kila wiki la Raia Mwema kwa siku 90. Na kama kuna gazeti lilijitahidi mno 'kumnadi' Magufuli ni Raia Mwema. Nakumbuka makala nyingi katika gazeti hilo wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi zilisheheni habari 'nzuri' kuhusu Magufuli. Pengine si vibaya nikitumia fursa hii kueleza kuwa sababu hasa iliyonifanya niache uandishi wa makala katika gazeti hilo ni kwamba lilihojiwa na 'vijana wa Magufuli' kuhusu mie lakini wahusika hawakuona umuhimu wa kunieleza wala kuandika kuhusu habari hiyo. Na kilichopelekea bwege huyo kudadisi kuhusu mie ni TWEET...Yes just a tweet a #FutureTweet to be precise. Kanuni muhimu katika chombo cha habari ni kwamba unyanyasaji wa taasisi yoyote ile dhidi ya mwenzenu ni unyanyasaji dhidi yenu nyote. Gazeti hilo lilipaswa kunijulisha kuhusu kilichotokea au kukiandika kama habari gazetini. Lakini bahati nzuri mie mzoefu wa 'dark arts' nikafahamu mapema kilichokuwa kinaendelea. Hata hivyo kitendo cha gazeti hilo nilikiona kama usaliti nikaamua kuachana nao. Hata hivyo mie sina kinyong'o nao na ndio maana jana nililaani na kupiga kelele kuhusu hatua hiyo ya serikali. Haya yanatokea wakati Tanzania bado ipo kwenye mshtuko kufuatia jaribio la kumuua mwanasiasa ambaye amekuwa mpinzani mkubwa wa Magufuli mbunge wa Chadema Tundu Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria cha TLS. Chuki inayopandikizwa dhidi ya wapinzani imepelekea takriban asilimia 99 ya viongozi wa CCM kuogopa kwenda kumjulia hali Lissu huko Nairobi alikolazwa. Lakini pengine kipimo halisi cha mambo kwenda kinyume na matarajio ya baadhi yetu kuhusu Magufuli ni kwamba tangu aingie madarakani zaidi ya viongozi na wanachama 400 wa Chadema wamekamatwa na polisi. Imefika mahala wakuu wa wilaya wanakamata viongozi wa Chadema kila wanapojisikia. Na pengine kibaya zaidi ni ukweli kwamba taratibu jamii inaanza kuzowea kuona viongozi na wanachama wa upinzani hususan Chadema wakidhalilishwa na kukamatwa kiholela. Jambo jingine la kusikitisha kuhusu utawala wa Magufuli ni utitiri wa sheria kandamizi kuhusu uhuru wa habari. Licha ya sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 ambayo ni kazi ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete tayari kuna sheria ya Huduma za Habari ambayo shujaa Nape alihusika kwa kiasi kikubwa na sasa kuna kinachoitwa Kanuni za Maudhui ya Mitandao ya Kijamii ambayo laiti zikipitishwa zitakuwa balaa kubwa. Na huku Chadema ikishuhudia viongozi na wanachama wake wakinyanyaswa ovyo ovyo kuna kila dalili kuwa mgogoro unaoendelea ndani ya chama cha CUF una mkono wa serikali hasa kwa kuzingatia mwenendo wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (taasisi ya serikali) kuibeba waziwazi kambi ya mwanachama aliyejiuzulu kwa utashi wake Prof Lipumba ambaye from nowhere alirudi chamani na kudai yeye bado mwenyekiti. Majuzi Magufuli katumwagia siri kwamba kuna siku aliombwa ushauri na Spika Ndugai kuhusu uteuzi wa wajumbe wa kamati ya bunge. Hiyo ina maana kuwa bunge limewekwa mfukoni na mhimili wa serikali. Kadhalika kauli za Jaji Mkuu mpya baada ya jaribio la mauaji dhidi ya Tundu Lissu zinajenga taswira ya mhimili wa mahakama nao kuwekwa mfukoni na mhimili wa serikali. Katika kuhitimisha makala hii ndefu ninarudia swali lililobeba kichwa cha habari: nini kilichomsibu Magufuli hadi kubadilika kiasi hiki? Kauli yake kuwa alisukumwa kuchukua fomu ya urais inazidi kuleta mkanganyiko kwamba labda alikuwa anafahamu fika hana uwezo wa kuongoza taifa letu lakini akakubali tu kutokana na shinikizo hilo ambalo hata hivyo hatujui limetoka kwa watu gani. Dalili kwamba Magufuli atabadilika (kurejea kuwa yule tuliyemwona ni mkombozi wetu) ni finyu. Kwa vile maamuzi yake mengi yanamtengenezea maadui zaidi ya waliopo kuna kila dalili kwamba atazidi kuwa mkali ili kujilinda. Tutegemee uhuru wa kujieleza/habari uendelee kubinywa zaidi kadri bwana mkubwa anavyozidi kutukumbusha yeye ndio Rais asiyeambiwa nini cha kufanya anayejua siri zote na nchi yetu na vitu kama hivyo. Nimalizie kwa kuwakumbusha Watanzania wenzangu kuhusu rai ya mara kwa mara ya Rais Magufuli kuwataka Watanzania tumwombee. Na tufanye hivyo kwa bidii kubwa ili Mwenyezi Mungu amwonyeshe njia sahihi ya kuliongoza taifa letu kwa kuzingatia haki na usawa. Tumwombee aondokane na 'fear of the unknown' apate muda wa kupumzika badala ya kukesha macho akihofia 'the unknown.' Aachane na chuki dhidi ya kila anayemkosoa hata kama kukosoa huko ni kwa nia njema. Tumwombee awe na busara ya kutokitumia 'kitengo' kama kampuni yake binafsi. Ajiulize kwanini licha ya ulinzi wake wa 'kufa mtu' bado siri zinavuja? Jibu jepesi: ukiwafanya watu wazima tena wenye utaalamu nyeti kuwa kama watoto inakuwa 'mwaga ugali nimwage mboga.' Na asije kukasirishwa na makala hii... Ni wazi kuwa ndoto za kuikomboa Tanzania yetu kiuchumi haziwezi kufanikiwa katika hali ya sasa ya siasa za vitisho kunyanyasa wapinzani watu wasiojulikana na vitu kama hivyo. Mungu ibariki Tanzania  JOHN MAGUFULI Leadership Models, Servant Leadership, Presidents In Order, Female Presidents, Nairobi, Julius Nyerere, Dodoma, African Nations
Uchambuzi Wa Kina: Nini Hasa Kimemfanya Magufuli Abadilike Kiasi Hiki?
Uchambuzi Wa Kina: Nini Hasa Kimemfanya Magufuli Abadilike Kiasi Hiki? Mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka juzi nilipata ujumbe kutoka kwa watu kadhaa wakinieleza kuwa kwa namna moja au nyingine niliwasaidia kufanya maamuzi ya kumpigia kura aliyekuwa mgombea wa CCM John Magufuli. Unajua moja ya makosa makubwa waliofanya wana-UKAWA kwenye kampeni za uchaguzi huo ni kutojihangaisha kulifikia kundi muhimu la wapigakura nchini Tanzania: wananchi wasiofungamana na chama chochote. Ili kulielewa vema kundi hili inabidi kuangalia idadi ya wanachama wa CCM na UKAWA (kwa kuzingatia uchaguzi wa mwaka 2015). Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa CCM ina wanachama milioni 8. Makadirio ya idadi ya wanachama wa UKAWA ni angalau milioni 5. Kwahiyo makadirio ya jumla ya wapigakura wenye kufungamana na vyama vya siasa ni takriban milioni 13. Tanzania ina watu zaidi ya milioni 50 tukitoa hao milioni 13 tunabakiwa na watu milioni 37. Tukienda kwenye idadi ya waliojiandikisha kupiga kura walikuwa milioni 23 hivi. Kwahiyo kimahesabu takriban watu milioni 10 (milioni 23 waliojiandikisha kutoa milioni 13 wenye ufuasi wa vyama vya siasa) walikuwa wapigakura wasiojihusisha na chama chochote. Tofauti na UKAWA ambayo viongozi na wanachama wake walielemea zaidi kuhamasishana wao kwa wao wenzao wa CCM waliwalenga hao takriban milioni 10 wasiofungamana na chama chochote. Na kimsingi mie japo sikuwa mpigakura nilikuwa katika kundi la watu wasio na vyama. Mara ya mwisho kuwa mwanachama wa chama cha siasa ilikuwa mwaka 2005 na takriban miaka 15 baadae sheria ilinizuwia kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Mwaka 2006 nilianza kufuatilia skandali ya Richmond iliyokuwa ikimhusisha aliyekuwa Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa. Naweza kwa uhakika kuwa nilikuwa bloga pekee niliyevalia njua suala hilo sambamba na kuliandikia makala mbalimbali katika magazeti ya Kulikoni na baadaye Mtanzania na hatimaye Raia Mwema. Ufuatiliaji huo ulinigharimu mno lakini hilo si la muhimu kwa sasa. Kutokana na bughudha niliyopata kuanzia mwaka 2006 na kuendelea haikuwa ajabu kwa mie kuunga mkono harakati za Chadema kupambana na ufisadi. Na mwaka 2010 nilishiriki kikamilifu kumnadi mgombea urais wa Chadema Dkt Wilbrord Slaa. Hata baada ya uchaguzi huo niliendelea kuunga mkono sera hiyo ya ufisadi ya Chadema.Hata hivyo sikuwahi kuwa mwanachama wa chama hicho. Mwanzoni mwa mwaka 2015 nilikuwa miongoni mwa watu waliopiga kelele kwenye mitandao ya kijamii kuwataka UKAWA watangaze mgombea wao wa kiti cha urais mapema hasa ikizingatiwa kuwa CCM walikuwa na safari ndefu ya kungoana macho kugombea kuteuliwa na chama chao kuwania urais. Hata hivyo kelele hizo hazikuzaa matunda na utetezi mkubwa ulikuwa UKAWA inajibidiisha kushughulikia daftari la wapigakura sambamba na kuhamasisha wapigakura watarajiwa kujiandikisha. Hatimaye tulikuja kufahamu kuwa mbinu hiyo ya kununua muda ililenga kumwandalia nafasi Bwana Lowassa endapo asingepitishwa huko CCM. Muungano wa vyama makini vinne vya upinzani unasubiri kapi kutoka chama tawala! Kufupisha stori mara baada ya UKAWA kumtangaza Lowassa kuwa mgombea wao kwa sie wengine ilikuwa haiwezekani tena kuunga mkono umoja huo uliojumuisha vyama vya Chadema CUF NCCR-Mageuzi na NLD. Kwa vile wagombea wakuu katika uchaguzi huo walikuwa Lowassa na Magufuli ilikuwa vigumu kumpinga Lowassa bila kumsapoti Magufuli. Kwahiyo japo awali nilijaribu kuepuka kumnadi mgombea wa CCM Magufuli mazingira yaliyokuwepo pamoja na mkataba wa kutoa huduma ya usadi (consultancy) ilipelekea nami nianze kumnadi Magufuli. Haukuwa uamuzi rahisi hasa kwa kuzingatia serikali ya CCM ilivyonitenda kuanzia mwaka 2006 nilipoanza kufuatilia skandali ya Richmond. Ushiriki wangu kwenye kampeni haukuwa rahisi. Katika maisha yangu yote sikuwahi kutukanwa kiasi nilichotukanwa katika kampeni za uchaguzi huo. Jitihada zangu za kuwaelewesha watu kwanini nimelazimika kumuunga mkono Magufuli hazikusaidia kitu. Pengine kibaya zaidi ni kwamba wakati wa kuelekea uchaguzi huo nilifiwa na baba yangu marehemu Mzee Philemon Chahali. Baadhi ya watu bila utu walitumia msiba huo kuingiza uhasama wa kisiasa. Pamoja na mvua ya matusi ya kila aina niliendelea na jukumu la kumnadi Bwana Magufuli. Nadhani mchango wangu mkubwa zaidi ulikuwa kwa wapigakura waliokuwa hawajafungama na chama chochote. Na nilifahamu kuhusu hilo baada ya uchaguzi ambapo baadhi yao walinieleza bayana kuwa ushawishi wangu kwao ulipelekea kufanya uamuzi wa kumpigia kura mgombea huyo wa CCM. Lakini tukiweka kando sababu zangu binafsi Magufuli alionekana kama mgombea bora zaidi ya mpinzani wake Lowassa. Pamoja na sababu nyingine wakati Magufuli alikuwa mgombea wa CCM kutoka CCM Lowassa alikuwa mgombea wa UKAWA kutoka CCM. Hatimaye uchaguzi ukafanyika na Magufuli akaibuka mshindi. Kama kuna kitu kilichonipa matumaini sana kuhusu urais wa Magufuli ni hotuba yake aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa bunge la Jamhuri ya Muungano. Katika hotuba hiyo Magufuli alionyesha kuwa mtu anayezielewa vema shida za Watanzania hususan janga la rushwa na ufisadi na akaapa kushughulikia kwa nguvu zake zote. Na alipoomba Watanzania wamwombee katika vita hiyo ngumu naamini hata miongoni mwa wale ambao hawakumpigia kura waliitikia wito huo wa kumfanyia maombi. Kisha zikaja ziara ya kushtukiza na taratibu tukaanza kuingiwa na matumaini mapya ya mrithi halisi wa Nyerere/Sokoine. Na dunia pia ikaungana nasi kusherehekea kiongozi huyo adimu na ikaibuka alama ya reli #WhatWouldMagufuli Do iliyotamba kila kona ya dunia. Na haikupita wiki bila kushuhudia tumbua majipu. Kwa kufurahishwa na kuridhishwa na utendaji wake mie nikajipinda na kuandika kitabu cha tathmini ya urais wa Magufuli siku 55 tu baada ya yeye kuapishwa kuwa Rais wa tano wa Tanzania. Watu kadhaa walinikosoa kwamba haikuwa sahihi kwangu kufanya tathmini hiyo mapema kiasi hicho. Kwa wakati huo niliona walionikosoa kuhusu suala hilo kama watu wenye chuki binafsi dhidi ya mkombozi Magufuli. Dalili ya kwanza kwamba huenda kuna walakini katika utawala wa Magufuli ni pale alipotangaza baraza lake la mawaziri ambalo ilituchukua wiki kadhaa kulisubiri. Lilipotangazwa sio tu lilikuwa kubwa kuliko ahadi yake kuwa angeunda serikali ndogo tu ili kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali bali pia lilijumuisha baadhi ya sura zenye utata. Miongoni mwa sura hizo ni Profesa Muhongo ambaye alilazimika kujiuzulu katika serikali ya Awamu ya Nne kutokana na kuhusishwa na skandali ya Tegeta Escrow. Kuna tuliouona uteuzi wa mtu kama Nape Nnauye kuwa ni wa kisiasa zaidi huku sura kama Simbachawene Lukuvi na Profesa Maghembe zikijenga ishara kuwa huenda mambo hayajabadilika kama tulivyotarajia. Kisha kukafanyika uteuzi wa mabalozi ambao ulionekana bayana kama kutumia nafasi hizo nyeti kuwaondoa watu flani kwenye nyadhifa zao huko CCM. Baadhi yetu tukaanza kujiuliza hivi hatujayashuhudia haya huko nyuma? Lakini tukaendelea kuwa na matumaini. Dalili ya kwanza kabisa kuwa pamoja na mazuri yake yaliyowavutia Watanzania wengi na kona mbalimbali duniani Bwana Magufuli ana mapungufu yake ni pale serikali yake kupitia shujaa wa sasa Nape Nnauye ilipozuwia haki ya mamilioni ya Watanzania kusikiliza matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. Niwe mkweli wanaomwona Nape shujaa huwa siwaelewi kabisa. Ningemwona shujaa laiti angetumia ukongwe wake ndani ya CCM kumweleza bosi wake Magufuli kuwa wazo la kuzuwia matangazo ya bunge live ni fyongo na laiti Magufuli angemomea basi angejiuzulu kishujaa badala ya kusubiri kufukuzwauwaziri kwa kupambana na kimeo kingine cha Magufuli yaani Daudi Albert Bashite. Baadaye likaja zuwio dhidi ya mikutano na maandamano ya vyama ya siasa. Awali baadhi yetu tulijipa matumaini kwamba ah huu ni muda wa kuchapa kazi. Hayo maandamano na mikutano ni ya nini muda huu? Kwahiyo kwa wakati huo ili-make sense. Mara tukakumbwa na janga la tetemeko la ardhi huko Kagera. Ikategemewa Rais angekwenda kuwafariji wahanga hasa ikizingatiwa kuwa anatoka Kanda ya Ziwa. Hakwenda hadi baadaye. Na alipokwenda akatoa hotuba isiyopendeza kuisikiliza. Maneno kama serikali haikuleta tetemeko la ardhi sio ya busara hata kidogo. Pia akaongopa kwa kudai hakuna serikali duniani inayotoa misaada kwa wahanga wa majanga ya asili. Sijui muda huu anajisikiaje akiona kwenye runinga jinsi serikali ya Marekani inavyowahudumia wahanga wa vimbunga. Baadaye kukusikika taarifa mbalimbali za tishio la uhaba wa chakula lakini badala ya kuwafariji wananchi Magufuli akawaropokea kwamba serikali yake haitotoa chakula kwa vile serikali haina shamba. Na wakati mmoja alipita sijui Nzega au Urambo mwananchi mmoja akamwambia njaa Mheshimiwa. Hilo jibu alilotoa utadhani ugomvi. Pamoja na majibu mengine ya ngebe akasema njaa kwani mnataka niingie jikoni kuwapikia? Ovyo kabisa. Likatokea tukio la maaskari polisi wanane kuuawa huko Kibiti lakini Amiri Jeshi Mkuu akaenda kufungua mabweni chuo kikuu cha Dar es Salaama badala ya kwenda kuaga miili ya askari hao. Pia kulijitokeza tukio la kupotea kwa kada wa Chadema Ben Saanane ambaye hadi kupotea kwake alikuwa akihoji kwa nguvu kubwa kuhusu PhD ya Magufuli. Baadhi tulimsihi awe makini (kwa sababu dalili zilishaanza kujionyesha kuwa Magufuli ni mtu wa aina gani) lakini bahati mbaya hakusikia ushauri wetu. Hadi leo haijulikani nini kimemsibu kijana huyo japo Chadema nao hawawezi kukwepa lawama katika poor handling ya suala hilo. Kumekuwa na kauli zinazokinzana kutoka kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho kama ile ya mwenyekiti Mbowe kuwa Ben alitekwa huku Mbunge wa chama hicho Saeid Kubenea akidai kuwa kada huyo anaonekana vijiweni. Kwanini chama hicho hakijawabana viongozi hao kufafanua kauli zao only God knows! Lakini kama kuna tukio lililompotezea heshima kubwa Bwana Magufuli ni lile la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kuvamia stesheni ya redio na runinga cha Clouds akiwa na askari wenye silaha. Siku chache baadaye huku baadhi ya watu wakitarajia angemtimua Makonda Magufuli akatufanya sote mabwege kwa kumtetea Makonda huku akidai yeye hapangiwi kazi yeye ndo Rais na kumwita Makonda mchapakazi. Yaani Mkuu wa Mkoa amevamia kituo cha habari kitendo ambacho ni kosa la jinai halafu Rais anamsifu kuwa ni mchapakazi? Uswahiba wa Magufuli na Makonda umechangia mno ugumu wa kuchunguza tuhuma kuwa mkuu huyo wa mkoa amefoji jina analotumia pamoja na cheti cha kuhitimu kidato cha nne. Laiti Magufuli angekuwa mwajibikaji kama tunavyoamini basi angeamuru uchunguzi kuhusu suala hilo. Na kwa wanaofahamu yanayoendelea nyuma ya pazia inadaiwa kuwa vetting aliyofanyiwa Bashite ilionyesha bayana mapungufu yanatajwa kumhusu yeye na Bwana mkubwa akashauriwa kuchukua hatua stahili lakini hakufuata ushauri huo. Hili la Bashite limeendelea kuwakera watu wengi sana hasa ikizingatiwa kuwa mtu huyo anatumia ipasavyo upendeleo anaopewa na Magufuli na kufanya dharau za wazi kama ile ya kupigiwa saluti na vingozi wa ngazi za juu wa jeshi la polisi huku amevaa kapelo. Hiyo ni dharau ya hali ya juu kwa vyombo vyetu vya dola. Na Magufuli ataingia kwenye vitabu vya historia kwa serikali yake kulifungia gazeti la kila wiki la Mwanahalisi kwa miaka mitatu na siku 10 baadaye akalifungia gazeti jingine la kila wiki la Raia Mwema kwa siku 90. Na kama kuna gazeti lilijitahidi mno 'kumnadi' Magufuli ni Raia Mwema. Nakumbuka makala nyingi katika gazeti hilo wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi zilisheheni habari 'nzuri' kuhusu Magufuli. Pengine si vibaya nikitumia fursa hii kueleza kuwa sababu hasa iliyonifanya niache uandishi wa makala katika gazeti hilo ni kwamba lilihojiwa na 'vijana wa Magufuli' kuhusu mie lakini wahusika hawakuona umuhimu wa kunieleza wala kuandika kuhusu habari hiyo. Na kilichopelekea bwege huyo kudadisi kuhusu mie ni TWEET...Yes just a tweet a #FutureTweet to be precise. Kanuni muhimu katika chombo cha habari ni kwamba unyanyasaji wa taasisi yoyote ile dhidi ya mwenzenu ni unyanyasaji dhidi yenu nyote. Gazeti hilo lilipaswa kunijulisha kuhusu kilichotokea au kukiandika kama habari gazetini. Lakini bahati nzuri mie mzoefu wa 'dark arts' nikafahamu mapema kilichokuwa kinaendelea. Hata hivyo kitendo cha gazeti hilo nilikiona kama usaliti nikaamua kuachana nao. Hata hivyo mie sina kinyong'o nao na ndio maana jana nililaani na kupiga kelele kuhusu hatua hiyo ya serikali. Haya yanatokea wakati Tanzania bado ipo kwenye mshtuko kufuatia jaribio la kumuua mwanasiasa ambaye amekuwa mpinzani mkubwa wa Magufuli mbunge wa Chadema Tundu Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria cha TLS. Chuki inayopandikizwa dhidi ya wapinzani imepelekea takriban asilimia 99 ya viongozi wa CCM kuogopa kwenda kumjulia hali Lissu huko Nairobi alikolazwa. Lakini pengine kipimo halisi cha mambo kwenda kinyume na matarajio ya baadhi yetu kuhusu Magufuli ni kwamba tangu aingie madarakani zaidi ya viongozi na wanachama 400 wa Chadema wamekamatwa na polisi. Imefika mahala wakuu wa wilaya wanakamata viongozi wa Chadema kila wanapojisikia. Na pengine kibaya zaidi ni ukweli kwamba taratibu jamii inaanza kuzowea kuona viongozi na wanachama wa upinzani hususan Chadema wakidhalilishwa na kukamatwa kiholela. Jambo jingine la kusikitisha kuhusu utawala wa Magufuli ni utitiri wa sheria kandamizi kuhusu uhuru wa habari. Licha ya sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 ambayo ni kazi ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete tayari kuna sheria ya Huduma za Habari ambayo shujaa Nape alihusika kwa kiasi kikubwa na sasa kuna kinachoitwa Kanuni za Maudhui ya Mitandao ya Kijamii ambayo laiti zikipitishwa zitakuwa balaa kubwa. Na huku Chadema ikishuhudia viongozi na wanachama wake wakinyanyaswa ovyo ovyo kuna kila dalili kuwa mgogoro unaoendelea ndani ya chama cha CUF una mkono wa serikali hasa kwa kuzingatia mwenendo wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (taasisi ya serikali) kuibeba waziwazi kambi ya mwanachama aliyejiuzulu kwa utashi wake Prof Lipumba ambaye from nowhere alirudi chamani na kudai yeye bado mwenyekiti. Majuzi Magufuli katumwagia siri kwamba kuna siku aliombwa ushauri na Spika Ndugai kuhusu uteuzi wa wajumbe wa kamati ya bunge. Hiyo ina maana kuwa bunge limewekwa mfukoni na mhimili wa serikali. Kadhalika kauli za Jaji Mkuu mpya baada ya jaribio la mauaji dhidi ya Tundu Lissu zinajenga taswira ya mhimili wa mahakama nao kuwekwa mfukoni na mhimili wa serikali. Katika kuhitimisha makala hii ndefu ninarudia swali lililobeba kichwa cha habari: nini kilichomsibu Magufuli hadi kubadilika kiasi hiki? Kauli yake kuwa alisukumwa kuchukua fomu ya urais inazidi kuleta mkanganyiko kwamba labda alikuwa anafahamu fika hana uwezo wa kuongoza taifa letu lakini akakubali tu kutokana na shinikizo hilo ambalo hata hivyo hatujui limetoka kwa watu gani. Dalili kwamba Magufuli atabadilika (kurejea kuwa yule tuliyemwona ni mkombozi wetu) ni finyu. Kwa vile maamuzi yake mengi yanamtengenezea maadui zaidi ya waliopo kuna kila dalili kwamba atazidi kuwa mkali ili kujilinda. Tutegemee uhuru wa kujieleza/habari uendelee kubinywa zaidi kadri bwana mkubwa anavyozidi kutukumbusha yeye ndio Rais asiyeambiwa nini cha kufanya anayejua siri zote na nchi yetu na vitu kama hivyo. Nimalizie kwa kuwakumbusha Watanzania wenzangu kuhusu rai ya mara kwa mara ya Rais Magufuli kuwataka Watanzania tumwombee. Na tufanye hivyo kwa bidii kubwa ili Mwenyezi Mungu amwonyeshe njia sahihi ya kuliongoza taifa letu kwa kuzingatia haki na usawa. Tumwombee aondokane na 'fear of the unknown' apate muda wa kupumzika badala ya kukesha macho akihofia 'the unknown.' Aachane na chuki dhidi ya kila anayemkosoa hata kama kukosoa huko ni kwa nia njema. Tumwombee awe na busara ya kutokitumia 'kitengo' kama kampuni yake binafsi. Ajiulize kwanini licha ya ulinzi wake wa 'kufa mtu' bado siri zinavuja? Jibu jepesi: ukiwafanya watu wazima tena wenye utaalamu nyeti kuwa kama watoto inakuwa 'mwaga ugali nimwage mboga.' Na asije kukasirishwa na makala hii... Ni wazi kuwa ndoto za kuikomboa Tanzania yetu kiuchumi haziwezi kufanikiwa katika hali ya sasa ya siasa za vitisho kunyanyasa wapinzani watu wasiojulikana na vitu kama hivyo. Mungu ibariki Tanzania JOHN MAGUFULI
Uchambuzi wa Kiintelijensia Kuhusu Jaribio la Kumuua Lissu: Wahusika Kina Nani ?  Jana Septemba 07 2017 majira ya mchana zilipatikana taarifa kwamba Tundu Lissu Mwanasheria Mkuu wa Chadema Mbunge wa Singida Mashariki Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS) amepigwa risasi kadhaa na kujeruhiwa vibaya. Tukio hilo la kutisha lilitokea jijini Dodoma wakati Mbunge huyo aliposhuka nyumbani kwake eneo la Area D inakoelezwa alienda kwa ajili ya kujipatia mlo wa mchana.  Kabla ya kuingia kiundani kwenye makala hii nitumie fursa hii kutoa salamu za pole kwa Lissu na kumwombea apone haraka. Salamu za pole pia kwa viongozi wanachama na wafuasi wa Chadema chama ambacho Lissu amekuwa akikiwakilisha kwa ufanisi mkubwa. Pia ni vema nitahadharishe mapema kwamba intelijensia sio sayansi timilifu kwa asilimia 100 kwa kimombo wanasema intelligence is not an exact science.  Okey sasa tuingie mtamboni. Hadi muda huu kuna dhana za msingi tatu ambazo zinatokana namchujo wa dhana mbalimbali. Dhana ya kwanza na ambayo pengine ni maarufu zaidi ya zote ni kwamba jaribio hilo la mauaji ya Lissu lina mkono wa dola. Kwamba sio siri kuwa Lissu amekuwa akiisumbua mno serikali ambapo wafuasi wake wanamwona kama jasiri asiye na uoga wa kusema ukweli ilhali wapinzani wake wakimwona kama mchochezi. Yayumkinika kuhitimisha kwamba kama kuna mwanasiasa wa upinzani ambaye amekuwa mwiba mchungu kwa serikali ya Rais John Magufuli basi si mwingine bali Lissu.  Na pengine kinachoongeza uzito kwenye dhana hii ni ukweli kwamba Agosti 18 mwaka huu Lissu aliwaeleza wananchi kwamba anafuatiliwa. Namnukuu "Naomba kabla sijaanza Mazungumzo yangu nimuombe Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Kipilimba au Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfululizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari ya Toyota premio namba T460CQV jana niliwakaba Kanisani St. Peter's. Kwa upande mwingine serikali ya Magufuli ni kama ilikuwa inatafuta kulaumiwa bure. Kwa sababu Hadi muda huu hakuna sababu moja ya msingi kwa serikali hiyo kuyafanya maisha ya wanasiasa wa upinzani yawe magumu kiasi hiki. Magumu kwa maana ya kuwanyima kila aina ya fursa ya kufanya siasa (political space).  Kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya viongozi na wafuasi 400 wa Chadema wameshakamatwa tangu Magufuli aingie madarakani. Mtu atayedai kuwa kiongozi huyo anawachukia wapinzani hatoonekana mtu wa ajabu japo huenda akatupwa jela. Katika hotuba zake mbalimbali Rais Magufuli ameshindwa kuficha hisia zake dhidi ya upinzani na wapinzani. Juni 12 mwaka huu Rais Magufuli alimweleza Spika Job Ndugai maneno yafuatayo  Tumia mbinu hiyohiyo ya kuwafanya wasiropokee Bungeni waropokee nje na kule tutadili nao vizuri kwasababu wanapokua kule ndani wana kinga wanaweza wakatukana chochote sasa kinga wanayoitumia vibaya bungeni kainyooshe wewe. Wawe wanatoka kule bungeni ukishamfukuza hata mwezi mzima atakuja aropokee huku na mimi nakueleza waache waropokee huku nitadili nao wala siwatishi lakini hatuwezi kuwa kwenye vita wewe unaanza kugeuka kupiga wale wanaokwenda mbele. ni nafuu unyamaze ukalale. Kwa kuangalia jinsi watendaji wa serikali ngazi za mkoa na wilaya wanavyochuana na polisi kuwanyanyasa wapinzani hususan wa Chadema dhana kuwa serikali ina mkono katika jaribio la mauaji ya Lissu ni kama ready-made. Hata hivyo pamoja na dalili zote kuashiria uwezekano wa mkono wa serikali katika jaribio la kumuua Lissu dhana hii inakosa mantiki kiuhalisia. Ni kwamba hakuna tija kwa serikali kumuua Lissu. Sawa sio siri kuwa uhusiano kati ya serikali na Lissu/ wapinzani sio mzuri lakini haitokuwa na tija yoyote kwa serikali ya Magufuli kumuua Lissu. Na hata kama ingekuwa lazima aondoke basi kuna njia mwafaka zaidi za mauaji ya watu maarufu (assassination) huku 'kifo cha ajali' ikiwa maarufu na rahisi zaidi. Halafu kinachotatiza katika tukio la jana na kinachopunguza zaidi nguvu ya dhana kwamba kuna mkono wa serikali ni jinsi waliofanya shambulio hilo walivyoonekana kama wanahitaji publicity ya kutosha. Kwanini? Jibu lipo kwenye uchambuzi wa dhana ya tatu. Dhana ya pili ni dhaifu kuliko nyingine mbili. Hii inahusisha mbio za urais mwaka 2020. Kwamba kila siku Lissu amekuwa akijitengenezea mazingira ya mgombea mwafaka wa Chadema/Upinzani katika uchaguzi mkuu ujao wala halina mjadala. Sio kwamba Lissu amekuwa hodari katika masuala mbalimbali kwa vile anataka urais (hajawahi kutamka nia ya kugombea nafasi hiyo) lakini umahiri wake bungeni na katika masuala ya kisheria na kitaifa kwa ujumla unamfanya kuwa kipenzi cha takriban kila mfuasi wa Chadema.  Dhana hii dhaifu inasema kuwa jaribio hilo la mauaji ni kazi ya wapinzani wa kisiasa wa Lissu hususan ndani ya chama chake.  Udhaifu wa dhana hii ni kwamba kama ambavyo kwenye dhana ya kwanza hakuna tija katika kumdhuru Lissu hadharani. Kwamba hata kama kungekuwa na lundo la wapinzani wa kisiasa wa Lissu huko kwenye chama chake kwanini wafanye operesheni hiyo waziwazi badala ya kuandaa mkakati wa siri? Na kama ilivyokuwa kwenye dhana ya kwanza hata kama wapinzani wa kisiasa wa Lissu ndani ya chama chake wangekuwa wahusika kwanini basi tukio hilo lifanyike katika mazingira ya kusaka publicity kwa nguvu? Hiyo inatuacha na dhana moja ya tatu na ya mwisho. Ya mwisho lakini sio haba katika mantiki. Dhana hii inaeleza kwamba jaribio hilo la mauaji limefanywa makusudi na kile wajuzi wa mambo wanaita rogue elements. Hizi zilitusumbua sana katika utawala wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete. Rogue elements hizi zinajumuisha watumishi halali wa vyombo vya dola wanaofanya shughuli zisizo halali. Nani anawatuma? Hiyo ni habari nyingine. Kuna kitu kinachofahamika kama Deep state. Kila nchi ina tafsiri yake kuhusu deep state lakini tafsiri nyepesi kwa mazingira yetu ni ushirika wa watu wenye nguvu katika serikali na jamii mfano vigogo (hususan wa zamani) wa vyombo vya dola wafanyabiashara wenye uwezo mkubwa na wanasiasa kutoka upande wowote ule lakini zaidi chama kilichopo madarakani. Dhana hii inaliona tukio la kujaribu kumuua Lissu kama njia rahisi ya kuichafua serikali ya Rais Magufuli ambayo kwa bahati mbaya/makusudi ilishajitengenezea mazingira ya kulaumiwa pindi la kutokea likimtokea mwanasiasa wa upinzani kama Lissu. Rais anaposhindwa kudhibiti chuki zake dhidi ya wapinzani anawapa nafasi nzuri wabaya wake kutenda kitu kisha ikawa rahisi tu lawama kuelekezwa kwake. Ndio maana dhana ya kwanza kwamba kuna mkono wa serikali ya Magufuli kwenye jaribio la kumuua Lissu inaonekana kama yenye uzito kwa vile "kuna sababu ready-made. Dhana hii inapata uzito kutokana na ukweli kwamba Magufuli amejitengenezea maadui wengi wenye nguvu na baadhi yao wakiwa viumbe hatari. Kuna watu waliozowea kuishi maisha ya kifalme ambao sasa wanalazimishwa kuishi maisha ya kawaida. Hawa watu wakipata upenyo wa kumdhuru Magufuli hawatosita kufanya hivyo. Lakini kwa vile ni vigumu mno (angalau kwa wakati huu) kufanikisha jaribio la kumdhuru kiongozi huyo njia nyepesi inaweza kuwa katika kuua character yake ambayo bahati nzuri kwa wabaya wake sio nzuri sana. Kumekuwa na malalamiko kadhaa hasa kutoka upande wa upinzani kumtuhumu Magufuli kuwa ni dikteta. Na ukifuatilia mwenendo wa siasa zetu kwa muda huu sio siri kwamba kuna chembe chembe za udikteta. Kwahiyo ni rahisi kwa wabaya wa Magufuli kutumia mwanya huo kujenga picha ya serikali ya dikteta yamuua mpinzani wake mkubwa.  Na hilo linatuleta kwenye suala la publicity. Kwamba jaribio la mauaji hayo liwe na mwangwi wa kutosha ndani na nje ya Tanzania. Mwangwi huo ni wa makusudi ili uakisi taswira inayojengeka kuwa Magufuli ni dikteta. Na madikteta hunyanyasa wapinzani wao na ikibidi hata kuwaua. Kwahiyo kama kuna funzo kubwa kwa Magufuli katika tukio hili ni kuepuka mazingira yaliyopo ya uhasama mkubwa dhidi ya upinzani hususan Chadema. Kiongozi huyo anatambua fika kwamba kuna watu wapo radhi kufanya lolote lile kumngoa na kwa vile njia za kawaida sio rahisi basi inakuwa anything goes liwalo na liwe. Na dhana hii ya tatu inaleta uhusiano kati ya tukio la jana la jaribio la kumuua Lissu na lile la hivi karibuni la kuchomwa moto kwa ofisi za kampuni ya uwakili wa IMMA. Kama hili la Lissu tukio la moto nalo lilifanyika katika mazingira ya kuvutia publicity yaani kama kulikuwa na jitihada za makusudi za kuushawishi umma kwamba mnaona huyu dikteta Magufuli anakoelekea? Sasa anachoma hadi ofisi wa wabaya wake. Nihitimishe uchambuzi huu kwa kueleza bayana masuala mawili matatu. Kwanza lengo la uchambuzi huu mfupi sio kuingilia kazi za vyombo vya dola vinavyoendelea na uchunguzi kuhusu jaribio la kumuua Lissu. Nimefanya uchambuzi huu kama mtu mwenye uelewa wa masuala ya intelijensia na siasa za Tanzania yetu ikiwa ni pamoja na yanayojiri nyuma ya pazia. Pili lengo la uchambuzi huu sio kumshawishi mtu yeyote abadili mtazamo wake kuhusu nani ana/wanahusika.  Mwisho kama nilivyotanabaisha awali tasnia ya intelijensia sio sayansi kamilifu kwa asilimia 100 (intelligence is not an exact science). Kwa maana hiyo japo uchambuzi huu ni karibu kabisa na hali halisi sio rahisi sana kufikia hali halisi yenye uhakika wa asilimia 100.  Nimalizie kwa kumtakia afya njema Bwana Lissu huku nikiamini kuwa malaka husika zitafanya kila jitihada kuwanasa wahusika sio tu kwa minajili ya serikali kujinasua bali ili Bwana Lissu atendewe haki.  TUNDU LISSU Exact Science, Kwanza, Hakuna, Lipo, Politics, Board, Planks
Uchambuzi wa Kiintelijensia Kuhusu Jaribio la Kumuua Lissu: Wahusika Kina Nani ?
Uchambuzi wa Kiintelijensia Kuhusu Jaribio la Kumuua Lissu: Wahusika Kina Nani ? Jana Septemba 07 2017 majira ya mchana zilipatikana taarifa kwamba Tundu Lissu Mwanasheria Mkuu wa Chadema Mbunge wa Singida Mashariki Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani na Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS) amepigwa risasi kadhaa na kujeruhiwa vibaya. Tukio hilo la kutisha lilitokea jijini Dodoma wakati Mbunge huyo aliposhuka nyumbani kwake eneo la Area D inakoelezwa alienda kwa ajili ya kujipatia mlo wa mchana. Kabla ya kuingia kiundani kwenye makala hii nitumie fursa hii kutoa salamu za pole kwa Lissu na kumwombea apone haraka. Salamu za pole pia kwa viongozi wanachama na wafuasi wa Chadema chama ambacho Lissu amekuwa akikiwakilisha kwa ufanisi mkubwa. Pia ni vema nitahadharishe mapema kwamba intelijensia sio sayansi timilifu kwa asilimia 100 kwa kimombo wanasema intelligence is not an exact science. Okey sasa tuingie mtamboni. Hadi muda huu kuna dhana za msingi tatu ambazo zinatokana namchujo wa dhana mbalimbali. Dhana ya kwanza na ambayo pengine ni maarufu zaidi ya zote ni kwamba jaribio hilo la mauaji ya Lissu lina mkono wa dola. Kwamba sio siri kuwa Lissu amekuwa akiisumbua mno serikali ambapo wafuasi wake wanamwona kama jasiri asiye na uoga wa kusema ukweli ilhali wapinzani wake wakimwona kama mchochezi. Yayumkinika kuhitimisha kwamba kama kuna mwanasiasa wa upinzani ambaye amekuwa mwiba mchungu kwa serikali ya Rais John Magufuli basi si mwingine bali Lissu. Na pengine kinachoongeza uzito kwenye dhana hii ni ukweli kwamba Agosti 18 mwaka huu Lissu aliwaeleza wananchi kwamba anafuatiliwa. Namnukuu "Naomba kabla sijaanza Mazungumzo yangu nimuombe Mkuu wa idara ya Usalama wa Taifa anaitwa Kipilimba au Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro wale vijana ambao wamewatuma na kwa wiki tatu mfululizo wananifuata kila nilipo wanaotembea na gari ya Toyota premio namba T460CQV jana niliwakaba Kanisani St. Peter's. Kwa upande mwingine serikali ya Magufuli ni kama ilikuwa inatafuta kulaumiwa bure. Kwa sababu Hadi muda huu hakuna sababu moja ya msingi kwa serikali hiyo kuyafanya maisha ya wanasiasa wa upinzani yawe magumu kiasi hiki. Magumu kwa maana ya kuwanyima kila aina ya fursa ya kufanya siasa (political space). Kwa mujibu wa takwimu zilizopo zaidi ya viongozi na wafuasi 400 wa Chadema wameshakamatwa tangu Magufuli aingie madarakani. Mtu atayedai kuwa kiongozi huyo anawachukia wapinzani hatoonekana mtu wa ajabu japo huenda akatupwa jela. Katika hotuba zake mbalimbali Rais Magufuli ameshindwa kuficha hisia zake dhidi ya upinzani na wapinzani. Juni 12 mwaka huu Rais Magufuli alimweleza Spika Job Ndugai maneno yafuatayo Tumia mbinu hiyohiyo ya kuwafanya wasiropokee Bungeni waropokee nje na kule tutadili nao vizuri kwasababu wanapokua kule ndani wana kinga wanaweza wakatukana chochote sasa kinga wanayoitumia vibaya bungeni kainyooshe wewe. Wawe wanatoka kule bungeni ukishamfukuza hata mwezi mzima atakuja aropokee huku na mimi nakueleza waache waropokee huku nitadili nao wala siwatishi lakini hatuwezi kuwa kwenye vita wewe unaanza kugeuka kupiga wale wanaokwenda mbele. ni nafuu unyamaze ukalale. Kwa kuangalia jinsi watendaji wa serikali ngazi za mkoa na wilaya wanavyochuana na polisi kuwanyanyasa wapinzani hususan wa Chadema dhana kuwa serikali ina mkono katika jaribio la mauaji ya Lissu ni kama ready-made. Hata hivyo pamoja na dalili zote kuashiria uwezekano wa mkono wa serikali katika jaribio la kumuua Lissu dhana hii inakosa mantiki kiuhalisia. Ni kwamba hakuna tija kwa serikali kumuua Lissu. Sawa sio siri kuwa uhusiano kati ya serikali na Lissu/ wapinzani sio mzuri lakini haitokuwa na tija yoyote kwa serikali ya Magufuli kumuua Lissu. Na hata kama ingekuwa lazima aondoke basi kuna njia mwafaka zaidi za mauaji ya watu maarufu (assassination) huku 'kifo cha ajali' ikiwa maarufu na rahisi zaidi. Halafu kinachotatiza katika tukio la jana na kinachopunguza zaidi nguvu ya dhana kwamba kuna mkono wa serikali ni jinsi waliofanya shambulio hilo walivyoonekana kama wanahitaji publicity ya kutosha. Kwanini? Jibu lipo kwenye uchambuzi wa dhana ya tatu. Dhana ya pili ni dhaifu kuliko nyingine mbili. Hii inahusisha mbio za urais mwaka 2020. Kwamba kila siku Lissu amekuwa akijitengenezea mazingira ya mgombea mwafaka wa Chadema/Upinzani katika uchaguzi mkuu ujao wala halina mjadala. Sio kwamba Lissu amekuwa hodari katika masuala mbalimbali kwa vile anataka urais (hajawahi kutamka nia ya kugombea nafasi hiyo) lakini umahiri wake bungeni na katika masuala ya kisheria na kitaifa kwa ujumla unamfanya kuwa kipenzi cha takriban kila mfuasi wa Chadema. Dhana hii dhaifu inasema kuwa jaribio hilo la mauaji ni kazi ya wapinzani wa kisiasa wa Lissu hususan ndani ya chama chake. Udhaifu wa dhana hii ni kwamba kama ambavyo kwenye dhana ya kwanza hakuna tija katika kumdhuru Lissu hadharani. Kwamba hata kama kungekuwa na lundo la wapinzani wa kisiasa wa Lissu huko kwenye chama chake kwanini wafanye operesheni hiyo waziwazi badala ya kuandaa mkakati wa siri? Na kama ilivyokuwa kwenye dhana ya kwanza hata kama wapinzani wa kisiasa wa Lissu ndani ya chama chake wangekuwa wahusika kwanini basi tukio hilo lifanyike katika mazingira ya kusaka publicity kwa nguvu? Hiyo inatuacha na dhana moja ya tatu na ya mwisho. Ya mwisho lakini sio haba katika mantiki. Dhana hii inaeleza kwamba jaribio hilo la mauaji limefanywa makusudi na kile wajuzi wa mambo wanaita rogue elements. Hizi zilitusumbua sana katika utawala wa Awamu ya Nne wa Rais Jakaya Kikwete. Rogue elements hizi zinajumuisha watumishi halali wa vyombo vya dola wanaofanya shughuli zisizo halali. Nani anawatuma? Hiyo ni habari nyingine. Kuna kitu kinachofahamika kama Deep state. Kila nchi ina tafsiri yake kuhusu deep state lakini tafsiri nyepesi kwa mazingira yetu ni ushirika wa watu wenye nguvu katika serikali na jamii mfano vigogo (hususan wa zamani) wa vyombo vya dola wafanyabiashara wenye uwezo mkubwa na wanasiasa kutoka upande wowote ule lakini zaidi chama kilichopo madarakani. Dhana hii inaliona tukio la kujaribu kumuua Lissu kama njia rahisi ya kuichafua serikali ya Rais Magufuli ambayo kwa bahati mbaya/makusudi ilishajitengenezea mazingira ya kulaumiwa pindi la kutokea likimtokea mwanasiasa wa upinzani kama Lissu. Rais anaposhindwa kudhibiti chuki zake dhidi ya wapinzani anawapa nafasi nzuri wabaya wake kutenda kitu kisha ikawa rahisi tu lawama kuelekezwa kwake. Ndio maana dhana ya kwanza kwamba kuna mkono wa serikali ya Magufuli kwenye jaribio la kumuua Lissu inaonekana kama yenye uzito kwa vile "kuna sababu ready-made. Dhana hii inapata uzito kutokana na ukweli kwamba Magufuli amejitengenezea maadui wengi wenye nguvu na baadhi yao wakiwa viumbe hatari. Kuna watu waliozowea kuishi maisha ya kifalme ambao sasa wanalazimishwa kuishi maisha ya kawaida. Hawa watu wakipata upenyo wa kumdhuru Magufuli hawatosita kufanya hivyo. Lakini kwa vile ni vigumu mno (angalau kwa wakati huu) kufanikisha jaribio la kumdhuru kiongozi huyo njia nyepesi inaweza kuwa katika kuua character yake ambayo bahati nzuri kwa wabaya wake sio nzuri sana. Kumekuwa na malalamiko kadhaa hasa kutoka upande wa upinzani kumtuhumu Magufuli kuwa ni dikteta. Na ukifuatilia mwenendo wa siasa zetu kwa muda huu sio siri kwamba kuna chembe chembe za udikteta. Kwahiyo ni rahisi kwa wabaya wa Magufuli kutumia mwanya huo kujenga picha ya serikali ya dikteta yamuua mpinzani wake mkubwa. Na hilo linatuleta kwenye suala la publicity. Kwamba jaribio la mauaji hayo liwe na mwangwi wa kutosha ndani na nje ya Tanzania. Mwangwi huo ni wa makusudi ili uakisi taswira inayojengeka kuwa Magufuli ni dikteta. Na madikteta hunyanyasa wapinzani wao na ikibidi hata kuwaua. Kwahiyo kama kuna funzo kubwa kwa Magufuli katika tukio hili ni kuepuka mazingira yaliyopo ya uhasama mkubwa dhidi ya upinzani hususan Chadema. Kiongozi huyo anatambua fika kwamba kuna watu wapo radhi kufanya lolote lile kumngoa na kwa vile njia za kawaida sio rahisi basi inakuwa anything goes liwalo na liwe. Na dhana hii ya tatu inaleta uhusiano kati ya tukio la jana la jaribio la kumuua Lissu na lile la hivi karibuni la kuchomwa moto kwa ofisi za kampuni ya uwakili wa IMMA. Kama hili la Lissu tukio la moto nalo lilifanyika katika mazingira ya kuvutia publicity yaani kama kulikuwa na jitihada za makusudi za kuushawishi umma kwamba mnaona huyu dikteta Magufuli anakoelekea? Sasa anachoma hadi ofisi wa wabaya wake. Nihitimishe uchambuzi huu kwa kueleza bayana masuala mawili matatu. Kwanza lengo la uchambuzi huu mfupi sio kuingilia kazi za vyombo vya dola vinavyoendelea na uchunguzi kuhusu jaribio la kumuua Lissu. Nimefanya uchambuzi huu kama mtu mwenye uelewa wa masuala ya intelijensia na siasa za Tanzania yetu ikiwa ni pamoja na yanayojiri nyuma ya pazia. Pili lengo la uchambuzi huu sio kumshawishi mtu yeyote abadili mtazamo wake kuhusu nani ana/wanahusika. Mwisho kama nilivyotanabaisha awali tasnia ya intelijensia sio sayansi kamilifu kwa asilimia 100 (intelligence is not an exact science). Kwa maana hiyo japo uchambuzi huu ni karibu kabisa na hali halisi sio rahisi sana kufikia hali halisi yenye uhakika wa asilimia 100. Nimalizie kwa kumtakia afya njema Bwana Lissu huku nikiamini kuwa malaka husika zitafanya kila jitihada kuwanasa wahusika sio tu kwa minajili ya serikali kujinasua bali ili Bwana Lissu atendewe haki. TUNDU LISSU
Uchambuzi Wa Kiintelijensia Kuhusu Mauaji Ya #MKIRU Kwa Kutumia "Dhana Zinazoshindana" (ACH)  Kabla ya kuingia kwa kina kwenye uchambuzi huu ni muhimu kueleza bayana kwamba japo maana mbinu na ufanisi wa uchambuzi wa kiintelijensia ('intelligence analysis' kwa kimombo) kati ya mie niliyepo hapa Glasgow na afisa mchambuzi wa intelijensia aliyepo Dar zaweza kuwa karibu na sawa mazingira kati yangu na ya afisa huyo ni tofauti. Tofauti sio kwa vile mie nipo Uingereza na afisa husika yupo Tanzania b Tanzania Music, Rubbish Dump, Madrasa, Guantanamo, Arusha, Music Promotion, Unidentified
Uchambuzi Wa Kiintelijensia Kuhusu Mauaji Ya #MKIRU Kwa Kutumia "Dhana Zinazoshindana" (ACH)
Uchambuzi Wa Kiintelijensia Kuhusu Mauaji Ya #MKIRU Kwa Kutumia "Dhana Zinazoshindana" (ACH) Kabla ya kuingia kwa kina kwenye uchambuzi huu ni muhimu kueleza bayana kwamba japo maana mbinu na ufanisi wa uchambuzi wa kiintelijensia ('intelligence analysis' kwa kimombo) kati ya mie niliyepo hapa Glasgow na afisa mchambuzi wa intelijensia aliyepo Dar zaweza kuwa karibu na sawa mazingira kati yangu na ya afisa huyo ni tofauti. Tofauti sio kwa vile mie nipo Uingereza na afisa husika yupo Tanzania b
Rugemalira Singasinga Kortini: JPM Amethubutu Tumuunge Mkono Katika Vita Hii  Katika Tanzania yetu ya zama hizi ambapo takriban kila jambo linaanglaiwa kwa jicho la kisiasa ni vigumu sio tu kusimamia ukweli bali pia kukwepa lawama kutoka kwa pande mbili kuu za siasa zetu: CCM au Upinzani. Sie tusio na vyama tukikosoa masuala yanayoigusa CCM/serikali akina Humphrey Polepole wanakurupuka na kutuita majina ya ajabu ajabu. Tukikosoa Upinzani tunaambiwa "nafasi za Ukuu wa Wilaya zimeshajaa." Good news is kuna watu - hata kama ni wachache - waliopo CCM Upinzani na wasio na vyama ambao wanatusikiliza. Na wanatusikiliza kwa vile wanafahamu hatuelemei upande wowote isipokuwa kwenye ukweli. Baada ya angalizo hilo tugeukia big news iliyosikika jana ghafla na kutukuta wengi wetu tusiamini macho/masikio yetu. Baada ya miaka nenda miaka rudi hatimaye mfanyabiashara James Rugemalira na mwenzie Singasinga Harbinder Seth Singh walipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuhujumu uchumi. Dear God let this be for real! https://t.co/Ond2iYs6d8  Evarist Chahali (@Chahali) June 19 2017 BREAKING: TAKUKURU imesema inawafikisha mahakamani watuhumiwa James Rugemarila na Harbinder Sethi wa IPTL kwa makosa ya Uhujumu Uchumi. http://pic.twitter.com/w5mhRVWM3E  Tanzania Updates (@TanzaniaUpdates) June 19 2017 Kwa tunaofahamu Rugemalira ameisumbua Tanzania yetu kiasi gani na sambamba na 'usumbufu' wa huyu Singasinga hatua hiyo tu ya kuwapindisha wawili hao kizimbani inastahili pongezi za kila Mtanzania. Na anayestahili pongezi hizo kwa wingi kabisa ni Rais John Magufuli. Sawa kuna watakaosema kuwa "lakini hiyo si ndio kazi ya Rais?" only if tukipuuzia ukweli kwamba Rugemalira alikuwa kama ameshindikana katika Awamu angalau mbili zilizopita ya Mkapa na Kikwete na ilikuwa kama huyu mtu kaachwa afanye apendacho katika kuihujumu nchi yetu. Nimesoma angalizo la mwanasiasa wa Chadema na mwanasheria nguli Tundu Lissu akitahadharisha kuhusu Rugemalira na Singasinga kwamba hao ni sehemu tu ya mtandao mkubwa wa ufisadi. Hata hivyo japo angalizo hilo ni muhimu haliondoi ukweli kwamba angalau JPM amethubutu sio tu kuwapandisha Rugemalira na Singasinga kizimbani bali pia kuwalaza rumande. Ni wazi kuwa vita hii ambayo Rais Magufuli ameivalia njuga sio rahisi. Sio tu kwa vile inahusisha watu wenye uwezo mkubwa kifedha bali pia kwa sababu pia inawagusa baadhi ya wanasiasa maarufu ndani ya chama chake cha CCM. Licha ya angalizo la Lissu kuna baadhi ya wananchi wanaotoa tahadhari 'kushangilia mapema kabla ya dakika 90.' Hawa pia wana hoja ya msingi hasa kwa kuzingatia mfano kama wa kesi ya Balozi Mahalu. Hata hivyo kuna haja ya kuwa na matumaini hasa ikizingatiwa kuwa JPM hafanyi anayofanya kwa shinikizo la mtu yeyote yule. Ni utashi wake tu. Angetaka kukaa kimya kusingekuwa na maandamano ya kumshinikiza achukue hatua. Kama ningekuwa na fursa ya kumshauri Rais Magufuli basi ningemwomba sana awekeze nguvu zaidi katika vita hii dhidi ya ufisadi ambayo kwa hakika inawaunganisha Watanzania wengi waliochoka kuona nchi yao ikigeuzwa shamba la bibi badala ya 'uhasama na wanasiasa wa Upinzani.' Kwa mfano jana kabla ya habari hiyo ya Rugemalira na Singasinga kufikishwa mahakamani na baadaye kutupwa rumande zilizpatikana taarifa kuhusu serikali kupitia jeshi la polisi 'kuwabughudhi' wanasiasa kadhaa wa Chadema ikiwa ni pamoja na kuzuwia ziara ya Waziri Mkuu wa zamani na kiognozi wa ngazi za juu Chadema Frederick Sumaye. @MagufuliJP Mheshimiwa what is going on? http://pic.twitter.com/5A8KenmNkG  Evarist Chahali (@Chahali) June 19 2017 Katika kipindi hiki cha vita ngumu dhidi ya mafisadi na ufisadi tunapaswa kuwa kitu kimoja. Si kwamba vyama vya upinzani viungane na CCM bali angalau tofauti zisizo na msingi ziepukwe na kubwa zaidi ni kupeuka uadui wa kisiasa. Nihitimishe kwa pointi moja muhimu kwamba japo tuna historia isiyopendeza kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi na japo ni kweli kuwa wanasheria wa serikali hawana rekodi nzuri kwenye kesi kubwa za serikali na vilevile japo ni kweli kuwa mara nyingi ukada umekuwa kikwazo kwa serikali kuchukua hatua stahili dhidi ya mafisadi wito wangu kwa Watanzania wenzangu ni kumuunga mkono Rais Magufuli kwani angalau ameonyesha dhamira ya kuchukua hatua stahili. Vilevile ni muhimu kutambua kuwa vita hii sio dhidi ya watu tu bali ni dhidi ya mfumo uliojengeka muda mrefu. Kwa maana hiyo japo tunatamani kuona watuhumiwa wote wakikamatwa na kupandishwa kizimbani ni muhimu tuwe na subira hasa ikizingatiwa kuwa kukurupusha mambo kunaweza kutupelekea kupoteza kesi dhidi ya 'maadui' wetu ambao kwa uweo wao mkubwa wa kifedha wataajiri wanasheria bora kabisa kuwatetea. MUNGU IBARIKI TANZANIA HARBINDER SINGH JAMES RUGEMALIRA JOHN MAGUFULI Tegeta Escrow Ufisadi Tanzania Big News, Good News, Escrow, Sakata, Humphrey, Mambo, Dear God
Rugemalira, Singasinga Kortini: JPM Amethubutu, Tumuunge Mkono Katika Vita Hii
Rugemalira Singasinga Kortini: JPM Amethubutu Tumuunge Mkono Katika Vita Hii Katika Tanzania yetu ya zama hizi ambapo takriban kila jambo linaanglaiwa kwa jicho la kisiasa ni vigumu sio tu kusimamia ukweli bali pia kukwepa lawama kutoka kwa pande mbili kuu za siasa zetu: CCM au Upinzani. Sie tusio na vyama tukikosoa masuala yanayoigusa CCM/serikali akina Humphrey Polepole wanakurupuka na kutuita majina ya ajabu ajabu. Tukikosoa Upinzani tunaambiwa "nafasi za Ukuu wa Wilaya zimeshajaa." Good news is kuna watu - hata kama ni wachache - waliopo CCM Upinzani na wasio na vyama ambao wanatusikiliza. Na wanatusikiliza kwa vile wanafahamu hatuelemei upande wowote isipokuwa kwenye ukweli. Baada ya angalizo hilo tugeukia big news iliyosikika jana ghafla na kutukuta wengi wetu tusiamini macho/masikio yetu. Baada ya miaka nenda miaka rudi hatimaye mfanyabiashara James Rugemalira na mwenzie Singasinga Harbinder Seth Singh walipandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuhujumu uchumi. Dear God let this be for real! https://t.co/Ond2iYs6d8 Evarist Chahali (@Chahali) June 19 2017 BREAKING: TAKUKURU imesema inawafikisha mahakamani watuhumiwa James Rugemarila na Harbinder Sethi wa IPTL kwa makosa ya Uhujumu Uchumi. http://pic.twitter.com/w5mhRVWM3E Tanzania Updates (@TanzaniaUpdates) June 19 2017 Kwa tunaofahamu Rugemalira ameisumbua Tanzania yetu kiasi gani na sambamba na 'usumbufu' wa huyu Singasinga hatua hiyo tu ya kuwapindisha wawili hao kizimbani inastahili pongezi za kila Mtanzania. Na anayestahili pongezi hizo kwa wingi kabisa ni Rais John Magufuli. Sawa kuna watakaosema kuwa "lakini hiyo si ndio kazi ya Rais?" only if tukipuuzia ukweli kwamba Rugemalira alikuwa kama ameshindikana katika Awamu angalau mbili zilizopita ya Mkapa na Kikwete na ilikuwa kama huyu mtu kaachwa afanye apendacho katika kuihujumu nchi yetu. Nimesoma angalizo la mwanasiasa wa Chadema na mwanasheria nguli Tundu Lissu akitahadharisha kuhusu Rugemalira na Singasinga kwamba hao ni sehemu tu ya mtandao mkubwa wa ufisadi. Hata hivyo japo angalizo hilo ni muhimu haliondoi ukweli kwamba angalau JPM amethubutu sio tu kuwapandisha Rugemalira na Singasinga kizimbani bali pia kuwalaza rumande. Ni wazi kuwa vita hii ambayo Rais Magufuli ameivalia njuga sio rahisi. Sio tu kwa vile inahusisha watu wenye uwezo mkubwa kifedha bali pia kwa sababu pia inawagusa baadhi ya wanasiasa maarufu ndani ya chama chake cha CCM. Licha ya angalizo la Lissu kuna baadhi ya wananchi wanaotoa tahadhari 'kushangilia mapema kabla ya dakika 90.' Hawa pia wana hoja ya msingi hasa kwa kuzingatia mfano kama wa kesi ya Balozi Mahalu. Hata hivyo kuna haja ya kuwa na matumaini hasa ikizingatiwa kuwa JPM hafanyi anayofanya kwa shinikizo la mtu yeyote yule. Ni utashi wake tu. Angetaka kukaa kimya kusingekuwa na maandamano ya kumshinikiza achukue hatua. Kama ningekuwa na fursa ya kumshauri Rais Magufuli basi ningemwomba sana awekeze nguvu zaidi katika vita hii dhidi ya ufisadi ambayo kwa hakika inawaunganisha Watanzania wengi waliochoka kuona nchi yao ikigeuzwa shamba la bibi badala ya 'uhasama na wanasiasa wa Upinzani.' Kwa mfano jana kabla ya habari hiyo ya Rugemalira na Singasinga kufikishwa mahakamani na baadaye kutupwa rumande zilizpatikana taarifa kuhusu serikali kupitia jeshi la polisi 'kuwabughudhi' wanasiasa kadhaa wa Chadema ikiwa ni pamoja na kuzuwia ziara ya Waziri Mkuu wa zamani na kiognozi wa ngazi za juu Chadema Frederick Sumaye. @MagufuliJP Mheshimiwa what is going on? http://pic.twitter.com/5A8KenmNkG Evarist Chahali (@Chahali) June 19 2017 Katika kipindi hiki cha vita ngumu dhidi ya mafisadi na ufisadi tunapaswa kuwa kitu kimoja. Si kwamba vyama vya upinzani viungane na CCM bali angalau tofauti zisizo na msingi ziepukwe na kubwa zaidi ni kupeuka uadui wa kisiasa. Nihitimishe kwa pointi moja muhimu kwamba japo tuna historia isiyopendeza kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi na japo ni kweli kuwa wanasheria wa serikali hawana rekodi nzuri kwenye kesi kubwa za serikali na vilevile japo ni kweli kuwa mara nyingi ukada umekuwa kikwazo kwa serikali kuchukua hatua stahili dhidi ya mafisadi wito wangu kwa Watanzania wenzangu ni kumuunga mkono Rais Magufuli kwani angalau ameonyesha dhamira ya kuchukua hatua stahili. Vilevile ni muhimu kutambua kuwa vita hii sio dhidi ya watu tu bali ni dhidi ya mfumo uliojengeka muda mrefu. Kwa maana hiyo japo tunatamani kuona watuhumiwa wote wakikamatwa na kupandishwa kizimbani ni muhimu tuwe na subira hasa ikizingatiwa kuwa kukurupusha mambo kunaweza kutupelekea kupoteza kesi dhidi ya 'maadui' wetu ambao kwa uweo wao mkubwa wa kifedha wataajiri wanasheria bora kabisa kuwatetea. MUNGU IBARIKI TANZANIA HARBINDER SINGH JAMES RUGEMALIRA JOHN MAGUFULI Tegeta Escrow Ufisadi Tanzania
#RipotiYaMchanga Uchambuzi Kuhusu TulikotokaTulipo Na Tuendako Na Nini Kifanyike  Kwanza bila kujali ukada wa CCM au Chadema au kutokuwa kada ni muhimu kutambua kuwa katika Tanzania yetu ya sasa na pengine katika nchi nyingi za Dunia ya Tatu alichofanya Rais John Magufuli kinastahili pongezi. Ofkoz alichofanya ni kazi yake tunamlipa mshahara kama Rais wetu ili atutumikie na uamuzi wa kuunda tume mbili zakufuatilia kuhusu usafirishaji wa mchanga wa madini ni sehemu ya kazi tuliyomwajiri aifa Comic Books, Comic Book Cover, Comics, Cartoons
#RipotiYaMchanga Uchambuzi Kuhusu Tulikotoka,Tulipo Na Tuendako, Na Nini Kifanyike
#RipotiYaMchanga Uchambuzi Kuhusu TulikotokaTulipo Na Tuendako Na Nini Kifanyike Kwanza bila kujali ukada wa CCM au Chadema au kutokuwa kada ni muhimu kutambua kuwa katika Tanzania yetu ya sasa na pengine katika nchi nyingi za Dunia ya Tatu alichofanya Rais John Magufuli kinastahili pongezi. Ofkoz alichofanya ni kazi yake tunamlipa mshahara kama Rais wetu ili atutumikie na uamuzi wa kuunda tume mbili zakufuatilia kuhusu usafirishaji wa mchanga wa madini ni sehemu ya kazi tuliyomwajiri aifa
Missing You So Much Mama: Kumbukumbu Ya Miaka 9 Ya Kifo cha Marehemu Mama Chahali  Mama mpendwailikuwa siku kama yale leomiaka tisa iliyopitauliondoka hapa duniani wakati tunakuhitaji sana. Japo miaka tisa inaweza kuonekana ni muda mrefu kusahau machungukwangu mwanao imeshindikana. Kila siku ya Mungu ninaposali kukuombea pumziko na raha ya milele huko ulipohujikuta napatwa na uchungu usioelezeka. Kwa kifupi mama mpendwa kila siku baada ya kifo chako-siku kama ya leo miaka minane iliyopitaimeendelea kuwa ni hudhuni na majonzi yasiyoelezeka. Mama mpendwa ulikuwa ni zaidi ya mama kwangu kwa mumeo marehemu Baba Mzee Chahali (aliyeungana nawe huko peponi mwaka juzi) na kwa wanao wote na ndugu na jamaa. Nakumbuka mwaka 2005 nilipokuja likizo nyumbani ulirukaruka kwa furaha ukanikumbatia na kunipakata mwanao ukaniandalia maji ya kuoga ukanifanya nijsikie kama mtoto mchanga. Sikujua kuwa furaha ile ya mzazi kumwona mwanae waliopoteana kitambo kidogo sintoipata tena maishani. Inaniuma sana. Marehemu mama akicheza siku ya harusi ya mwanae wa nne. Yeye na marehemu baba walijaliwa kupata watoto tisa mmojaalifariki na tukabaki wanane wanaume sita na wanawake wawili. Nakumbuka wakati huo ambapo wewe na marehemu Baba mlikuwa mnasherehekea miaka 50 ya ndoa yenu ulinipa mafundisho mengi kuhusu maisha ndoa upendo na zaidi ni kumweka mbele Mungu katika kila ninalofanya. Kabla ya kifo chako nilikuwa nauangalia mkanda niliowarekodi wewe na marehemu Baba na kila nilipofanya hivyo niligundua kuwa nina bahati ya pekee kuwa na wazazi wanaonipenda kiasi hicho. Sikujua kuwa mahojiano yale ndio ulikuwa wosia wako na marehemu baba kwangu mwanenu. Kwa sasa sina nguvu ya kuangalia video hiyo kwani kila nikijaribu naishia kububujikwa na machozi. Nakumbua nilipokwenda chumba cha maiti na kukuona umelazwa kwenye zile friji wanzohifadhia maiti. Nilikugusa mama nilitaraji muujiza kwamba ungeamka na ndoto ile mbaya ingeisha. Hukuamka hadi leo hii. Hospitali Teule ya Mtakatifu Fransisko ambapo marehemu mama alilazwa akiwa amepoteza fahamu kwa zaidi ya miezi mitatu hadi alipofariki siku kama ya leo miaka minane iliyopita Mamainaniuma sana kwani nilipokuja kukuuguza Februari 2008 ulikuwa umeshapoteza fahamu. Ulipokuwa Muhimbili na baadaye St Francis Ifakaranilikuwa najaribu kukusemesha. Kama vile ulifahamu mwanao nimekuja kukuuguza kuna nyakati ulikuwa unatoa tabasamu lako lenye mwanya ulionirithisha. Nikategemea ungemka na kunieleza japo neno moja. Kwa bahati mbaya hadi unafariki hukuweza kuniambia chochote. Iliniuma sana inaniuma sana na itaendelea kuniuma sana mama. Kabla marehemu baba hajaungana nawe huko uliko nilikuwa na wakati mgumu sana kila nilipopiga simu nyumbani kwa wakati wa uhai wako nilizowea kuwa nikimaliza kuongea na Baba anakupa simu wewe tupige stori. Na kila nilipoongea nawe nilijisikia kudeka kutokana na upendo wako usiomithilika. Baada ya kifo chako na kabla marehemu baba hajafariki kila nilipompigia simu mzee huwa nilijikuta najisahau na nataka kumwambia Mzee akupe simu niongee nawekisha nakumbuka kuwa hauko nasi. Sasa ndio imekuwa uchungu maradufu kwani kila nikipiga simu nyumbani ninatamani kuongea nawe na marehemu baba kisha nakumbuka kuwa hampo nasi. Nyakati nyingine baadhi ya watu wangu wa karibu (ninao wengi kutokana na malezi bora uliyonipatia) huwa wananiona kama dhaifu ninapowaeleza uchungu nnilio nao takriban kila siku tangu ufariki wewe na baadaye marehemu baba. Siwalaumu kwani wanachojitahidi kufanya ni kunishawishi nikubali ukweli kuwa hampo nasi na haiwezekani kuwarejesha. Kuna wakati wananichukiza kwani najihisi kama hawaelewi jinsi kifo chako na cha baba vinavyoniathiri.Lakini baadaye akili hunirejea na kutambua wanachofanya ni kujaribu kunisaidia tu. Mama mpendwa sijui nisemeje. Rafiki zako wakubwa wanao vitinda-mimba Kulwa na Doto ndio wananitia uchungu zaidi Wanawa-miss mno wewe na marehemu baba kwa sababu ndio uhusiano wenu ulikuwa zaidi ya kati ya wazazi na vitinda-mimba wao. Nakumbuka siku zile nawapigia simu na kuwasikia mnacheka mnataniana na kunipa kila aina ya faraja. Kwa sasa imebaki kumbukumbu tu. Mama mpendwasiku ya mazishi yako Padre alituambia maneno haya: "Mama Adelina alikuwa mtu wa watu na kila anayemjua anafahamu hilo. Japo mnaomboleza kifo chake lakini mnapaswa kupata faraja kuwa kutokana na matendo yake mema Baba Yake wa Mbinguni Ameamua kumchukua. Sote tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi na ndio maana amemchukua." Maneno hayo ndio nguvu pekee inayonisaidia kumudu kufanya mambo mengine maishani. Nguvu nyingine niliyonanyo ni imani kuwa wewe na marehemu baba mnaendelea kutuombea huko mlipo. Nyumba ya milele ya marehemu Adelina Basi naomba nikuage tena mama kwa kumwomba BWANA AKUPATIE WEWE NA MAREHEMU BABA PUMZIKO LA MILELE NA MWANGA WA MILELE AWAANGAZIE MPUMZIKE KWA AMANI AMEEN. ADELINA MAPANGO Wako, Kila, Katy, Miss You, Miss, Yale, Dear Mom, Missing You So Much
Missing You So Much Mama: Kumbukumbu Ya Miaka 9 Ya Kifo cha Marehemu Mama Chahali
Missing You So Much Mama: Kumbukumbu Ya Miaka 9 Ya Kifo cha Marehemu Mama Chahali Mama mpendwailikuwa siku kama yale leomiaka tisa iliyopitauliondoka hapa duniani wakati tunakuhitaji sana. Japo miaka tisa inaweza kuonekana ni muda mrefu kusahau machungukwangu mwanao imeshindikana. Kila siku ya Mungu ninaposali kukuombea pumziko na raha ya milele huko ulipohujikuta napatwa na uchungu usioelezeka. Kwa kifupi mama mpendwa kila siku baada ya kifo chako-siku kama ya leo miaka minane iliyopitaimeendelea kuwa ni hudhuni na majonzi yasiyoelezeka. Mama mpendwa ulikuwa ni zaidi ya mama kwangu kwa mumeo marehemu Baba Mzee Chahali (aliyeungana nawe huko peponi mwaka juzi) na kwa wanao wote na ndugu na jamaa. Nakumbuka mwaka 2005 nilipokuja likizo nyumbani ulirukaruka kwa furaha ukanikumbatia na kunipakata mwanao ukaniandalia maji ya kuoga ukanifanya nijsikie kama mtoto mchanga. Sikujua kuwa furaha ile ya mzazi kumwona mwanae waliopoteana kitambo kidogo sintoipata tena maishani. Inaniuma sana. Marehemu mama akicheza siku ya harusi ya mwanae wa nne. Yeye na marehemu baba walijaliwa kupata watoto tisa mmojaalifariki na tukabaki wanane wanaume sita na wanawake wawili. Nakumbuka wakati huo ambapo wewe na marehemu Baba mlikuwa mnasherehekea miaka 50 ya ndoa yenu ulinipa mafundisho mengi kuhusu maisha ndoa upendo na zaidi ni kumweka mbele Mungu katika kila ninalofanya. Kabla ya kifo chako nilikuwa nauangalia mkanda niliowarekodi wewe na marehemu Baba na kila nilipofanya hivyo niligundua kuwa nina bahati ya pekee kuwa na wazazi wanaonipenda kiasi hicho. Sikujua kuwa mahojiano yale ndio ulikuwa wosia wako na marehemu baba kwangu mwanenu. Kwa sasa sina nguvu ya kuangalia video hiyo kwani kila nikijaribu naishia kububujikwa na machozi. Nakumbua nilipokwenda chumba cha maiti na kukuona umelazwa kwenye zile friji wanzohifadhia maiti. Nilikugusa mama nilitaraji muujiza kwamba ungeamka na ndoto ile mbaya ingeisha. Hukuamka hadi leo hii. Hospitali Teule ya Mtakatifu Fransisko ambapo marehemu mama alilazwa akiwa amepoteza fahamu kwa zaidi ya miezi mitatu hadi alipofariki siku kama ya leo miaka minane iliyopita Mamainaniuma sana kwani nilipokuja kukuuguza Februari 2008 ulikuwa umeshapoteza fahamu. Ulipokuwa Muhimbili na baadaye St Francis Ifakaranilikuwa najaribu kukusemesha. Kama vile ulifahamu mwanao nimekuja kukuuguza kuna nyakati ulikuwa unatoa tabasamu lako lenye mwanya ulionirithisha. Nikategemea ungemka na kunieleza japo neno moja. Kwa bahati mbaya hadi unafariki hukuweza kuniambia chochote. Iliniuma sana inaniuma sana na itaendelea kuniuma sana mama. Kabla marehemu baba hajaungana nawe huko uliko nilikuwa na wakati mgumu sana kila nilipopiga simu nyumbani kwa wakati wa uhai wako nilizowea kuwa nikimaliza kuongea na Baba anakupa simu wewe tupige stori. Na kila nilipoongea nawe nilijisikia kudeka kutokana na upendo wako usiomithilika. Baada ya kifo chako na kabla marehemu baba hajafariki kila nilipompigia simu mzee huwa nilijikuta najisahau na nataka kumwambia Mzee akupe simu niongee nawekisha nakumbuka kuwa hauko nasi. Sasa ndio imekuwa uchungu maradufu kwani kila nikipiga simu nyumbani ninatamani kuongea nawe na marehemu baba kisha nakumbuka kuwa hampo nasi. Nyakati nyingine baadhi ya watu wangu wa karibu (ninao wengi kutokana na malezi bora uliyonipatia) huwa wananiona kama dhaifu ninapowaeleza uchungu nnilio nao takriban kila siku tangu ufariki wewe na baadaye marehemu baba. Siwalaumu kwani wanachojitahidi kufanya ni kunishawishi nikubali ukweli kuwa hampo nasi na haiwezekani kuwarejesha. Kuna wakati wananichukiza kwani najihisi kama hawaelewi jinsi kifo chako na cha baba vinavyoniathiri.Lakini baadaye akili hunirejea na kutambua wanachofanya ni kujaribu kunisaidia tu. Mama mpendwa sijui nisemeje. Rafiki zako wakubwa wanao vitinda-mimba Kulwa na Doto ndio wananitia uchungu zaidi Wanawa-miss mno wewe na marehemu baba kwa sababu ndio uhusiano wenu ulikuwa zaidi ya kati ya wazazi na vitinda-mimba wao. Nakumbuka siku zile nawapigia simu na kuwasikia mnacheka mnataniana na kunipa kila aina ya faraja. Kwa sasa imebaki kumbukumbu tu. Mama mpendwasiku ya mazishi yako Padre alituambia maneno haya: "Mama Adelina alikuwa mtu wa watu na kila anayemjua anafahamu hilo. Japo mnaomboleza kifo chake lakini mnapaswa kupata faraja kuwa kutokana na matendo yake mema Baba Yake wa Mbinguni Ameamua kumchukua. Sote tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi na ndio maana amemchukua." Maneno hayo ndio nguvu pekee inayonisaidia kumudu kufanya mambo mengine maishani. Nguvu nyingine niliyonanyo ni imani kuwa wewe na marehemu baba mnaendelea kutuombea huko mlipo. Nyumba ya milele ya marehemu Adelina Basi naomba nikuage tena mama kwa kumwomba BWANA AKUPATIE WEWE NA MAREHEMU BABA PUMZIKO LA MILELE NA MWANGA WA MILELE AWAANGAZIE MPUMZIKE KWA AMANI AMEEN. ADELINA MAPANGO
#RipotiYaMchanga CCM Haiwezi Kukwepa Lawama Katika Ujambazi wa Utoroshaji Madini Yetu  Juzi tumesikia ripoti kuhusu mchanga wenye madini unaosafirishwa nje ya Tanzania yetu (well kuna jina la kitaalamu lakini sio la muhimu kulinganisha na athari kubwa za usafirishwaji wa mchanga huo). Kwa baadhi ya wenzetu taarifa hiyo imewashtua mno na kuwapandisha hasira kubwa. Ndio Tanzania yetu hiyo wengi wa raia wake hawana habari kuhusu yanayoisibu nchi yetu. Ukiwauliza watu "hivi mustakabali wa Tanzania
#RipotiYaMchanga CCM Haiwezi Kukwepa Lawama Katika Ujambazi wa Utoroshaji Madini Yetu
#RipotiYaMchanga CCM Haiwezi Kukwepa Lawama Katika Ujambazi wa Utoroshaji Madini Yetu Juzi tumesikia ripoti kuhusu mchanga wenye madini unaosafirishwa nje ya Tanzania yetu (well kuna jina la kitaalamu lakini sio la muhimu kulinganisha na athari kubwa za usafirishwaji wa mchanga huo). Kwa baadhi ya wenzetu taarifa hiyo imewashtua mno na kuwapandisha hasira kubwa. Ndio Tanzania yetu hiyo wengi wa raia wake hawana habari kuhusu yanayoisibu nchi yetu. Ukiwauliza watu "hivi mustakabali wa Tanzania
Baada Ya Takriban Miaka 20 ya Uandishi wa Makala Magazetini Nimeamua Kustaafu  Baada ya safari ya muda mrefu iliyodumu takriban miaka 20 sasa ya uandishi wa makala magazetini hatimaye nimeamua kutundika daluga (kustaafu) Nilianza rasmi uandishi mwaka 1998 nilipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mlimani. Aliyenishawishi kuingia kwenye fani hiyo ni aliyekuwa mwandishi mkongwe Albert Memba ambaye alidai kuwa nina kipaji cha asili cha kuandika. Nilianza uandishi katika gazeti la kwanza kabisa la udaku lililokuwa linajulikana kwa jina la "Sanifu." Gazeti hili lilikuwa maarufu sana na mpaka leo sijui kwanini halikudumu muda mrefu. Wakati nikiwa 'Sanifu' sikuwa nikiandika makala as such bali nilikuwa na safu yangu iliyohusu unajimu well sio kama ule wa Marehemu Sheikh Yahya lakini karibu kidogo. Ulikuwa utani wa aina flani ambao baadhi ya watu waliuchukulia serious. Na kama 'kachumbari' ninajipa jina la 'Ustaadh Bonge.' Na hadi leo baadhi ya marafiki zangu wa enzi za Mlimani (UDSM) wananiita jina hilo. Baadaye nikapata kolamu katika gazeti jipya la 'Kasheshe.' Hili lilikuwa gazeti la pili nchini Tanzania lililohusu udaku. Na huko nako nilikuwa na safu inayohusu unajimu nikiendelea na jina la 'Ustaadh Bonge.' Nilikuwa nikifarijika kila nilipomsikia marehemu Julius Nyaisanga akieleza wasomaji watarajie nini kwenye toleo la wiki husika la gazeti la Kasheshe huku akiwakumbusha "bila kusahau safu ya unajimu ya Ustaadh Bonge." Sema enzi hizo hata neno "kiki" lilikuwa halijazaliwa. Na kuna watu ambao baada ya mie kujitambulisha walipatwa na mshangao na kusema "ah mie nilijua Ustaadh Bonge ni mzee flani wa pwani..." na mie nikiishia kucheka tu. Baadaye tena nikapata safu kwenye gazeti-dada la 'Kasheshe' lililoitwa 'Komesha' ambako pia niliendelea na 'unajimu' wangu nikitumia jina lilelile la Ustaadh Bonge. Hatimaye likaanzishwa gazeti jipya la habari na makala lililojulikana kwa jina la 'Kulikoni.' Na hili ndilo hasa lililopelekea kuzaliwa kwa jina la blogu hii yaani 'Kulikoni Ughaibuni.' Blogu hii ilianzishwa kwa lengo la kuwa sehemua mabyo Watanzania walio nje ya nchi wangeweza kusoma makala zangu zilizochapaishwa katika gazeti la 'Kulikoni' lakini hazikuwepo mtandaoni kwa vile gazeti hilo halikuwa na tovuti. Kumbuka wakati huko kulikuwa hakuna Facebook wala Twitter wala Instagram wala selfie...hizo zilikuwa zama za Hi5 Myspace na kwa Tanzania kulikuwa na blogu chache tu na mtandao maarufu wa DarHotWire. Anyway kwa vile nilikuwa nakabiliwa na majukumu mbalimbali ilibidi niachane na uandishi katika magazeti ya udaku na kukazania uandishi wa makala. Safu yangu katika gazeti la 'Kulikoni' ilikuwa ikijulikana kama 'Kulikoni Ughaibuni.' Baadaye kidogo nikapata safu kwenye gazeti la Mtanzania nikaipa jina 'Mtanzania Ughaibuni' kabla ya kuanzishwa kwa gazeti la Raia Mwema ambako nilikuwa miongoni mwa wana-makala wa awali kabisa na safu yangu ikijulikana kama 'Raia Mwema Ughaibuni.' Moja ya matukio ambayo sintoyasahu katika uandishi wa makala ni uamuzi wangu wa kuvalia njuga sakata la Richmond. Licha ya kujivunia kama mwana-makala pekee niliyevalia njuga suala hilo vya kutosha athari zake zilikuwa kubwa mno. Kilichotokea wakati huo ndio kilichonisukuma kumuunga mkono mgombea wa CCM kwenye nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 John Magufuli. Uandishi wa makala ulinikuta nikikumbana na 'msala' mwingine mwaka 2013 ambapo mwanzoni mwa mwezi Februari (mwaka huo) nilijulishwa na vyombo vya dola hapa Uingereza kuwa kulikuwa maisha yangu yalikuwa hatarini. Kwahiyo hadi kufikia uamuzi wa kustaafu uandishi wa makala magazetini ni takriban miaka 20 sasa (actually ni miaka 19 yaani 2017 kutoa 1998). Nikipima 'faida' na 'hasara' za uandishi wa makala hizo jibu ni rahisi kabisa: faida zilizidi hasara. Ndio uandishi wa makala hizo umenigharimu mno kimaisha lakini ndani kabisa ya nafsi yangu ninaamini kuwa uamuzi wangu kuwasemea wasio na sauti (to be the voice of the voiceless) ulikuwa uamuzi sahihi. Ninaamini ilikuwa sahihi kusimama kidete kuhusu skandali ya Richmond tangu mwanzo hadi mwisho licha ya gharama kubwa kimaisha kwa upande wangu. Ninaamini nilikuwa sahihi kwa safu zangu kuwa sauti adimu iliyopigania haja ya mageuzi katika Idara ya Usalama wa Taifa kwa minajili ya kuondoa siasa katika utendaji kazi wa taasisi hiyo muhimu kuhamasisha uzalendo na kwa ujumla kubaki kuwa chombo muhimu kwa ustawi wa Tanzania yetu. Uandishi wa makala umenitengenezea marafiki wengi mno japo pia umenitengenezea maadui wachache wenye nguvu kisiasa au kijamii. Na jana nilipotoa taarifa rasmi huko Facebook nilipata fursa adimu ya kufahamu kuwa kumbe kuna idadi kubwa tu ya watu waliovutiwa na makala zangu. Uamuzi wangu kustaafu uandishi wa makala magazetini hauhusiani na 'yaliyonikumba wiki hii inayoisha leo.' Kwa upande mmoja nilipewa taarifa na ushahidi kuwa Rais Magufuli hakupendezwa na makala yangu ya mwisho katika gazeti la Raia Mwema ambayo ndani yake nilimkosoa kuwa "yeye kama Amiri Jeshi mkuu ni mfariji mkuu pia na anapaswa kuhudhuria misiba ya kitaifa." Japo kumkosoa kwangu hakukuwa tofauti na kauli ya Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambapo kiongozi huyo wa Chadema alieleza bayana kushangazwa kwake na hatua ya Rais kutohudhuria msiba wa wanafunzi 32 wa shule ya Lucky Vncent ya Arusha akisisitiza kwamba ni msiba mzito kitaifa ambao ilipaswa Rais kuhudhuria. Wakati kauli ya Lowassa ilijibiwa na Ikulu mie makala yangu imepelekea msala ambao nitauelezea siku nyingine. Kwa upande mwingine kuna watu waliohojiwa kuhusiana na tweet ya utani niliyoandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Ni kwamba katika 'mila na desturi' za Twitter kuna kitu kinaitwa 'future tweet' ambacho huandikwa kama alama ya reli #FutureTweet. Kitu hicho hutumika kama utani unaoashirika kuwa 'sikuzijazo kutakuwa na tweet ya aina hii baada ya kitu hiki kutokea.' Ni UTANI usiopaswa kuipotezea muda serikali sio tu kuandika taarifa rasmi za kuukanusha na kuahidi kuchukua hatua bali pia kuhoji watu kadhaa kuhusu mie mwandishi wa #FutureTweet hiyo. Huu ni UTOTO. Serikali ilioingia madarakani kwa mbwembwe za #HapaNiKaziTu inaonekana kioja kwa sio tu kushindwa kuelewa #FutureTweet ni kitu gani bali pia kituko kwa kufikia hatua ya kukanusha #FutureTweet na hatimaye kuhoji watu kuhusu mie mwandishi wa #FutureTweet hiyo. Niwe mkweli sikupendezwa na gazeti la Raia Mwema kutonijulisha kuwa walihojiwa kuhusu mie na kisha kutonambia kuhusu suala hilo. Kama walifanya hivyo kwa sababu ya uoga wao au waliamriwa kunificha binafsi nimetafsiri kama 'wameninyima ushirikiano' na sioni umuhimu wa kuendelea kuwa mwana-makala katika gazeti hilo. Lakini kubwa zaidi sitaki kuwasababishia usumbufu wasiostahili. Ungetegemea gazeti kubwa kama hilo lingepata ujasiri kuzungumzia kadhi hiyo ya kubughudhiwa na serikali kwa ajili yangu lakini ni wazi kuwa vyombo vyetu vya habari vimetishwa na tishio la Rais Magufuli kuwa "visidhani vina uhuru kiasi hicho." Nihitimishe makala hii kwa kuwashukuru nyote mliosoma makala zangu mbalimbali katika miaka hii takriban 20 ya utumishi wangu kwenu. Naomba ifahamike kuwa kustaafu kuandika makala magazetini hakumaanishi kuwa nimestaafu pia katika kublogu. Hapana. Na pia haimaanishi nimestaafu kuwa muumini wa #SharingIsCaring. Nitaendelea kutumia mitandao ya kijamii kuelimisha kuhabarisha kukosoa...na pengine kuburudisha. Nimeitumikia Tanzania yangu vya kutosha. Licha ya takriban miaka 20 ya uandishi wa makala niliitumia Tanzania yangu kwa uadilifu mkubwa kama mtumishi wa serikali na pia kupitia #SharingAndCaring na kublogu na uandishi wa vitabu.Lakini kubwa zaidi ni kwa kuwa raia mwema ambaye licha ya kuwa mbali na nchi yangu nimejitahidi kuwatumikia Watanzania wenzangu angalau kwa kushiriki mijadala muhimu kuhusu mustakabali wa taifa letu. Licha ya kuwa nitaendelea kublogu kuandika vitabu na kudumisha #SharingAndCaring kwenye mitandao ya kijamii kustaafu uandishi wa makala magazetini kunanipa fursa ya kuanza safari mpya ya maisha yangu: kuzalisha 'waleta mabadiliko wa kesho' (future change makers) kupitia ujasiriamali jamii (social entreprenuership).  Kustaafu Uandishi wa Makala Magazetini Dar Es Salaam, Chuo, Albert, 20th, Selfie, Selfies
Baada Ya Takriban Miaka 20 ya Uandishi wa Makala Magazetini Nimeamua Kustaafu
Baada Ya Takriban Miaka 20 ya Uandishi wa Makala Magazetini Nimeamua Kustaafu Baada ya safari ya muda mrefu iliyodumu takriban miaka 20 sasa ya uandishi wa makala magazetini hatimaye nimeamua kutundika daluga (kustaafu) Nilianza rasmi uandishi mwaka 1998 nilipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mlimani. Aliyenishawishi kuingia kwenye fani hiyo ni aliyekuwa mwandishi mkongwe Albert Memba ambaye alidai kuwa nina kipaji cha asili cha kuandika. Nilianza uandishi katika gazeti la kwanza kabisa la udaku lililokuwa linajulikana kwa jina la "Sanifu." Gazeti hili lilikuwa maarufu sana na mpaka leo sijui kwanini halikudumu muda mrefu. Wakati nikiwa 'Sanifu' sikuwa nikiandika makala as such bali nilikuwa na safu yangu iliyohusu unajimu well sio kama ule wa Marehemu Sheikh Yahya lakini karibu kidogo. Ulikuwa utani wa aina flani ambao baadhi ya watu waliuchukulia serious. Na kama 'kachumbari' ninajipa jina la 'Ustaadh Bonge.' Na hadi leo baadhi ya marafiki zangu wa enzi za Mlimani (UDSM) wananiita jina hilo. Baadaye nikapata kolamu katika gazeti jipya la 'Kasheshe.' Hili lilikuwa gazeti la pili nchini Tanzania lililohusu udaku. Na huko nako nilikuwa na safu inayohusu unajimu nikiendelea na jina la 'Ustaadh Bonge.' Nilikuwa nikifarijika kila nilipomsikia marehemu Julius Nyaisanga akieleza wasomaji watarajie nini kwenye toleo la wiki husika la gazeti la Kasheshe huku akiwakumbusha "bila kusahau safu ya unajimu ya Ustaadh Bonge." Sema enzi hizo hata neno "kiki" lilikuwa halijazaliwa. Na kuna watu ambao baada ya mie kujitambulisha walipatwa na mshangao na kusema "ah mie nilijua Ustaadh Bonge ni mzee flani wa pwani..." na mie nikiishia kucheka tu. Baadaye tena nikapata safu kwenye gazeti-dada la 'Kasheshe' lililoitwa 'Komesha' ambako pia niliendelea na 'unajimu' wangu nikitumia jina lilelile la Ustaadh Bonge. Hatimaye likaanzishwa gazeti jipya la habari na makala lililojulikana kwa jina la 'Kulikoni.' Na hili ndilo hasa lililopelekea kuzaliwa kwa jina la blogu hii yaani 'Kulikoni Ughaibuni.' Blogu hii ilianzishwa kwa lengo la kuwa sehemua mabyo Watanzania walio nje ya nchi wangeweza kusoma makala zangu zilizochapaishwa katika gazeti la 'Kulikoni' lakini hazikuwepo mtandaoni kwa vile gazeti hilo halikuwa na tovuti. Kumbuka wakati huko kulikuwa hakuna Facebook wala Twitter wala Instagram wala selfie...hizo zilikuwa zama za Hi5 Myspace na kwa Tanzania kulikuwa na blogu chache tu na mtandao maarufu wa DarHotWire. Anyway kwa vile nilikuwa nakabiliwa na majukumu mbalimbali ilibidi niachane na uandishi katika magazeti ya udaku na kukazania uandishi wa makala. Safu yangu katika gazeti la 'Kulikoni' ilikuwa ikijulikana kama 'Kulikoni Ughaibuni.' Baadaye kidogo nikapata safu kwenye gazeti la Mtanzania nikaipa jina 'Mtanzania Ughaibuni' kabla ya kuanzishwa kwa gazeti la Raia Mwema ambako nilikuwa miongoni mwa wana-makala wa awali kabisa na safu yangu ikijulikana kama 'Raia Mwema Ughaibuni.' Moja ya matukio ambayo sintoyasahu katika uandishi wa makala ni uamuzi wangu wa kuvalia njuga sakata la Richmond. Licha ya kujivunia kama mwana-makala pekee niliyevalia njuga suala hilo vya kutosha athari zake zilikuwa kubwa mno. Kilichotokea wakati huo ndio kilichonisukuma kumuunga mkono mgombea wa CCM kwenye nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 John Magufuli. Uandishi wa makala ulinikuta nikikumbana na 'msala' mwingine mwaka 2013 ambapo mwanzoni mwa mwezi Februari (mwaka huo) nilijulishwa na vyombo vya dola hapa Uingereza kuwa kulikuwa maisha yangu yalikuwa hatarini. Kwahiyo hadi kufikia uamuzi wa kustaafu uandishi wa makala magazetini ni takriban miaka 20 sasa (actually ni miaka 19 yaani 2017 kutoa 1998). Nikipima 'faida' na 'hasara' za uandishi wa makala hizo jibu ni rahisi kabisa: faida zilizidi hasara. Ndio uandishi wa makala hizo umenigharimu mno kimaisha lakini ndani kabisa ya nafsi yangu ninaamini kuwa uamuzi wangu kuwasemea wasio na sauti (to be the voice of the voiceless) ulikuwa uamuzi sahihi. Ninaamini ilikuwa sahihi kusimama kidete kuhusu skandali ya Richmond tangu mwanzo hadi mwisho licha ya gharama kubwa kimaisha kwa upande wangu. Ninaamini nilikuwa sahihi kwa safu zangu kuwa sauti adimu iliyopigania haja ya mageuzi katika Idara ya Usalama wa Taifa kwa minajili ya kuondoa siasa katika utendaji kazi wa taasisi hiyo muhimu kuhamasisha uzalendo na kwa ujumla kubaki kuwa chombo muhimu kwa ustawi wa Tanzania yetu. Uandishi wa makala umenitengenezea marafiki wengi mno japo pia umenitengenezea maadui wachache wenye nguvu kisiasa au kijamii. Na jana nilipotoa taarifa rasmi huko Facebook nilipata fursa adimu ya kufahamu kuwa kumbe kuna idadi kubwa tu ya watu waliovutiwa na makala zangu. Uamuzi wangu kustaafu uandishi wa makala magazetini hauhusiani na 'yaliyonikumba wiki hii inayoisha leo.' Kwa upande mmoja nilipewa taarifa na ushahidi kuwa Rais Magufuli hakupendezwa na makala yangu ya mwisho katika gazeti la Raia Mwema ambayo ndani yake nilimkosoa kuwa "yeye kama Amiri Jeshi mkuu ni mfariji mkuu pia na anapaswa kuhudhuria misiba ya kitaifa." Japo kumkosoa kwangu hakukuwa tofauti na kauli ya Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambapo kiongozi huyo wa Chadema alieleza bayana kushangazwa kwake na hatua ya Rais kutohudhuria msiba wa wanafunzi 32 wa shule ya Lucky Vncent ya Arusha akisisitiza kwamba ni msiba mzito kitaifa ambao ilipaswa Rais kuhudhuria. Wakati kauli ya Lowassa ilijibiwa na Ikulu mie makala yangu imepelekea msala ambao nitauelezea siku nyingine. Kwa upande mwingine kuna watu waliohojiwa kuhusiana na tweet ya utani niliyoandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Ni kwamba katika 'mila na desturi' za Twitter kuna kitu kinaitwa 'future tweet' ambacho huandikwa kama alama ya reli #FutureTweet. Kitu hicho hutumika kama utani unaoashirika kuwa 'sikuzijazo kutakuwa na tweet ya aina hii baada ya kitu hiki kutokea.' Ni UTANI usiopaswa kuipotezea muda serikali sio tu kuandika taarifa rasmi za kuukanusha na kuahidi kuchukua hatua bali pia kuhoji watu kadhaa kuhusu mie mwandishi wa #FutureTweet hiyo. Huu ni UTOTO. Serikali ilioingia madarakani kwa mbwembwe za #HapaNiKaziTu inaonekana kioja kwa sio tu kushindwa kuelewa #FutureTweet ni kitu gani bali pia kituko kwa kufikia hatua ya kukanusha #FutureTweet na hatimaye kuhoji watu kuhusu mie mwandishi wa #FutureTweet hiyo. Niwe mkweli sikupendezwa na gazeti la Raia Mwema kutonijulisha kuwa walihojiwa kuhusu mie na kisha kutonambia kuhusu suala hilo. Kama walifanya hivyo kwa sababu ya uoga wao au waliamriwa kunificha binafsi nimetafsiri kama 'wameninyima ushirikiano' na sioni umuhimu wa kuendelea kuwa mwana-makala katika gazeti hilo. Lakini kubwa zaidi sitaki kuwasababishia usumbufu wasiostahili. Ungetegemea gazeti kubwa kama hilo lingepata ujasiri kuzungumzia kadhi hiyo ya kubughudhiwa na serikali kwa ajili yangu lakini ni wazi kuwa vyombo vyetu vya habari vimetishwa na tishio la Rais Magufuli kuwa "visidhani vina uhuru kiasi hicho." Nihitimishe makala hii kwa kuwashukuru nyote mliosoma makala zangu mbalimbali katika miaka hii takriban 20 ya utumishi wangu kwenu. Naomba ifahamike kuwa kustaafu kuandika makala magazetini hakumaanishi kuwa nimestaafu pia katika kublogu. Hapana. Na pia haimaanishi nimestaafu kuwa muumini wa #SharingIsCaring. Nitaendelea kutumia mitandao ya kijamii kuelimisha kuhabarisha kukosoa...na pengine kuburudisha. Nimeitumikia Tanzania yangu vya kutosha. Licha ya takriban miaka 20 ya uandishi wa makala niliitumia Tanzania yangu kwa uadilifu mkubwa kama mtumishi wa serikali na pia kupitia #SharingAndCaring na kublogu na uandishi wa vitabu.Lakini kubwa zaidi ni kwa kuwa raia mwema ambaye licha ya kuwa mbali na nchi yangu nimejitahidi kuwatumikia Watanzania wenzangu angalau kwa kushiriki mijadala muhimu kuhusu mustakabali wa taifa letu. Licha ya kuwa nitaendelea kublogu kuandika vitabu na kudumisha #SharingAndCaring kwenye mitandao ya kijamii kustaafu uandishi wa makala magazetini kunanipa fursa ya kuanza safari mpya ya maisha yangu: kuzalisha 'waleta mabadiliko wa kesho' (future change makers) kupitia ujasiriamali jamii (social entreprenuership). Kustaafu Uandishi wa Makala Magazetini
Makala Yangu RAIA MWEMA 10.05.17: Si Sahihi Rais Kutoonekana Katika Misiba Ya Kitaifa  NIANZE makala hii kwa salamu za pole na rambirambi kwa ndugu jamaa na marafiki wa wanafunzi zaidi ya 30 waliopoteza maisha kufuatia ajali ya basi dogo la abiria huko Karatu Arusha. Nimeandika zaidi ya mara 30 kwa sababu wakati ninaandika makala hii zimepatikana taarifa kuwa inawezekana idadi ya abiria kwenye basi lililopata ajali ilikuwa kubwa kuliko iliyoripotiwa. Taarifa rasmi zinatajwa idadi ya waliofariki kuwa ni wanafunzi 33 walimu wawili na dereva mmoja. Mungu awapatie marehemu wote pumziko la milele na mwanga wa milele awaangazie wapumzike kwa amani. Amina. Bwana ametoa Bwana ametwaa. Wenzetu wametutangulia tu lakini sote tupo safari moja kwani kila nafsi huonja mauti. Salamu nyingi za pole kwa wafiwa maana uchungu wa mwana aujuaye mzazi. Wanafunzi hao wamekumbwa na mauti wakati wanaelekea kwenye mitihani yao. Kwa hiyo tunaomboleza sio kifo tu bali pia kukatishwa kwa ndoto za kielimu za wanafunzi hao. Hili ni pigo kubwa sio kwa ndugu jamaa na marafiki tu wa wanafunzi hao bali taifa kwa ujumla. Kwa mujibu wa mila na desturi zetu si vema kuanza kulaumiana kuhusu msiba kabla hata mazishi hayajafanyika. Lakini kama kuna kasumba mbaya inayojitokeza katika kila majanga makubwa kitaifa basi binafsi sioni haja ya kuwa na subira. Kama kuna kitu kinanisumbua mno kila yanapojiri majanga ya kitaifa kama ajali hii ya Karatu ni ile hali kwamba wenzetu huku nilipo wanathamini mno uhai uliopotea pengine kuliko sisi. Hili nimekwishaliongelea mara kadhaa na kuna mifano lukuki ya kuthibitisha hisia hizo zisizopendeza. Nashindwa kupata picha hali ingekuwaje hapa Uingereza laiti kungetokea ajali kama hiyo ya Karatu. Naandika hivyo kwa sababu ajali ndogo tu kwa maana ya idadi ya vifo au majeruhi hupewa uzito mkubwa mno kiasi kwamba takriban kila mkazi wa nchi hii anaguswa na janga husika. Nabaki ninajiuliza je wenzetu wanathamini mno uhai kuliko sisi? Sipati jawabu. Najiuliza tena labda wenzetu ni wazima lakini sisi tumerogwa? Siambulii jibu. Lakini kilicho wazi ni kwamba tuna upungufu mkubwa katika kuguswa kwetu na majanga makubwa kitaifa. Mifano ya karibuni zaidi ni janga la tetemeko la ardhi lililoyakumba maeneo ya Kanda ya Ziwa na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa na uharibifu mkubwa wa mali; mauaji dhidi ya askari polisi wanane huko Kibiti mkoani Pwani na sasa janga hili ambalo limeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani. Kitu kimoja kisichopendeza katika matukio yote hayo matatu ni kwamba serikali haikuona haja ya kutangaza maombolezo ya kitaifa. Katika udadisi wangu nimesikia utetezi usio na mashiko kuwa ili kuwe na maombolezo ya kitaifa na bendera ipepe nusu mlingoti basi msiba husika shurti uwe wa kiongozi wa kitaifa. Maana yake kwamba uhai wa viongozi wetu una thamani zaidi ya uhai wa wananchi wa kawaida. Ama? Kitu kingine ambacho sio tu hakipendezi lakini pia kinashangaza ni Rais wetu John Magufuli kutoungana na waombolezaji wakati wa kuaga miili ya marehemu. Hakuwepo katika tukio la kuaga miili ya waliofariki kwenye Tetemeko la Kagera hakuwepo kwenye tukio la kuaga miili ya askari polisi wanane waliouawa huko mkoani Pwani. Na hadi wakati naandika makala hii mgeni rasmi kwenye kuaga miili ya wanafunzi hao wa Karatu ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. Kuna wanaoweza kusema kwani rais akiwepo atarejesha uhai wa waliofariki? Hoja hiyo ni ya kukosa ubinadamu. Ni muhimu kutambua kuwa licha ya kuwa commander-in-chief wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama Rais pia ni comforter-in-chief. Rais ni kama baba mlezi na mtu ambaye taifa zima linamuangalia katika nyakati kama hizi. Tukiweka kando sintofahamu hiyo Shirika la Utangazaji la taifa TBC limeonyesha kasoro kwa kuendelea na ratiba za vipindi vyake badala ya kuongoza vyombo vingine vya habari katika maombolezo ya vifo vilivyotokana na ajali hiyo ya Karatu. Nitumie fursa hii kuipongeza Clouds Media Group kwa uzalendo na ubinadamu wao mkubwa uliowasukuma kubadili ratiba za vipindi vyao ili kuungana na wafiwa na Watanzania kwa ujumla kuomboleza vifo hivyo. Mwisho japo ajali haina kinga uzoefu unaonyesha kuwa ajali nyingi zinazotokea huko nyumbani huchangiwa na uzembe wa madereva ikiwa ni pamoja na kukiuka kwa makusudi kanuni za usalama barabarani sambamba na ubovu wa vyombo vya usafiri wa abiria. Japo sina maana kuwa sababu hizo ndio zilizochangia ajali hiyo ya Karatu lakini ni muhimu sasa kama taifa kuliangalia balaa la ajali kama janga la kitaifa. Kwa kiasi kikubwa madereva wazembe wapo barabarani huku wengine wakiendesha magari yasiyopaswa kuwa barabarani kwa sababu moja kuu ugonjwa sugu wa rushwa kwenye kitengo cha polisi wa usalama barabarani. Pasipo kukabili rushwa kwenye kitengo hicho uhai wetu utazidi kuwa mashakani kwa janga la ajali. Poleni sana wafiwa poleni Watanzania kwa ujumla. Njia mwafaka ya kuomboleza msiba huu mkubwa ni kwa kuwakumbuka marehemu katika dua/sala zetu RAIA MWEMA Sis, Blazer, 10 Things, Blazers
Makala Yangu RAIA MWEMA 10.05.17: Si Sahihi Rais Kutoonekana Katika Misiba Ya Kitaifa
Makala Yangu RAIA MWEMA 10.05.17: Si Sahihi Rais Kutoonekana Katika Misiba Ya Kitaifa NIANZE makala hii kwa salamu za pole na rambirambi kwa ndugu jamaa na marafiki wa wanafunzi zaidi ya 30 waliopoteza maisha kufuatia ajali ya basi dogo la abiria huko Karatu Arusha. Nimeandika zaidi ya mara 30 kwa sababu wakati ninaandika makala hii zimepatikana taarifa kuwa inawezekana idadi ya abiria kwenye basi lililopata ajali ilikuwa kubwa kuliko iliyoripotiwa. Taarifa rasmi zinatajwa idadi ya waliofariki kuwa ni wanafunzi 33 walimu wawili na dereva mmoja. Mungu awapatie marehemu wote pumziko la milele na mwanga wa milele awaangazie wapumzike kwa amani. Amina. Bwana ametoa Bwana ametwaa. Wenzetu wametutangulia tu lakini sote tupo safari moja kwani kila nafsi huonja mauti. Salamu nyingi za pole kwa wafiwa maana uchungu wa mwana aujuaye mzazi. Wanafunzi hao wamekumbwa na mauti wakati wanaelekea kwenye mitihani yao. Kwa hiyo tunaomboleza sio kifo tu bali pia kukatishwa kwa ndoto za kielimu za wanafunzi hao. Hili ni pigo kubwa sio kwa ndugu jamaa na marafiki tu wa wanafunzi hao bali taifa kwa ujumla. Kwa mujibu wa mila na desturi zetu si vema kuanza kulaumiana kuhusu msiba kabla hata mazishi hayajafanyika. Lakini kama kuna kasumba mbaya inayojitokeza katika kila majanga makubwa kitaifa basi binafsi sioni haja ya kuwa na subira. Kama kuna kitu kinanisumbua mno kila yanapojiri majanga ya kitaifa kama ajali hii ya Karatu ni ile hali kwamba wenzetu huku nilipo wanathamini mno uhai uliopotea pengine kuliko sisi. Hili nimekwishaliongelea mara kadhaa na kuna mifano lukuki ya kuthibitisha hisia hizo zisizopendeza. Nashindwa kupata picha hali ingekuwaje hapa Uingereza laiti kungetokea ajali kama hiyo ya Karatu. Naandika hivyo kwa sababu ajali ndogo tu kwa maana ya idadi ya vifo au majeruhi hupewa uzito mkubwa mno kiasi kwamba takriban kila mkazi wa nchi hii anaguswa na janga husika. Nabaki ninajiuliza je wenzetu wanathamini mno uhai kuliko sisi? Sipati jawabu. Najiuliza tena labda wenzetu ni wazima lakini sisi tumerogwa? Siambulii jibu. Lakini kilicho wazi ni kwamba tuna upungufu mkubwa katika kuguswa kwetu na majanga makubwa kitaifa. Mifano ya karibuni zaidi ni janga la tetemeko la ardhi lililoyakumba maeneo ya Kanda ya Ziwa na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa na uharibifu mkubwa wa mali; mauaji dhidi ya askari polisi wanane huko Kibiti mkoani Pwani na sasa janga hili ambalo limeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani. Kitu kimoja kisichopendeza katika matukio yote hayo matatu ni kwamba serikali haikuona haja ya kutangaza maombolezo ya kitaifa. Katika udadisi wangu nimesikia utetezi usio na mashiko kuwa ili kuwe na maombolezo ya kitaifa na bendera ipepe nusu mlingoti basi msiba husika shurti uwe wa kiongozi wa kitaifa. Maana yake kwamba uhai wa viongozi wetu una thamani zaidi ya uhai wa wananchi wa kawaida. Ama? Kitu kingine ambacho sio tu hakipendezi lakini pia kinashangaza ni Rais wetu John Magufuli kutoungana na waombolezaji wakati wa kuaga miili ya marehemu. Hakuwepo katika tukio la kuaga miili ya waliofariki kwenye Tetemeko la Kagera hakuwepo kwenye tukio la kuaga miili ya askari polisi wanane waliouawa huko mkoani Pwani. Na hadi wakati naandika makala hii mgeni rasmi kwenye kuaga miili ya wanafunzi hao wa Karatu ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. Kuna wanaoweza kusema kwani rais akiwepo atarejesha uhai wa waliofariki? Hoja hiyo ni ya kukosa ubinadamu. Ni muhimu kutambua kuwa licha ya kuwa commander-in-chief wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama Rais pia ni comforter-in-chief. Rais ni kama baba mlezi na mtu ambaye taifa zima linamuangalia katika nyakati kama hizi. Tukiweka kando sintofahamu hiyo Shirika la Utangazaji la taifa TBC limeonyesha kasoro kwa kuendelea na ratiba za vipindi vyake badala ya kuongoza vyombo vingine vya habari katika maombolezo ya vifo vilivyotokana na ajali hiyo ya Karatu. Nitumie fursa hii kuipongeza Clouds Media Group kwa uzalendo na ubinadamu wao mkubwa uliowasukuma kubadili ratiba za vipindi vyao ili kuungana na wafiwa na Watanzania kwa ujumla kuomboleza vifo hivyo. Mwisho japo ajali haina kinga uzoefu unaonyesha kuwa ajali nyingi zinazotokea huko nyumbani huchangiwa na uzembe wa madereva ikiwa ni pamoja na kukiuka kwa makusudi kanuni za usalama barabarani sambamba na ubovu wa vyombo vya usafiri wa abiria. Japo sina maana kuwa sababu hizo ndio zilizochangia ajali hiyo ya Karatu lakini ni muhimu sasa kama taifa kuliangalia balaa la ajali kama janga la kitaifa. Kwa kiasi kikubwa madereva wazembe wapo barabarani huku wengine wakiendesha magari yasiyopaswa kuwa barabarani kwa sababu moja kuu ugonjwa sugu wa rushwa kwenye kitengo cha polisi wa usalama barabarani. Pasipo kukabili rushwa kwenye kitengo hicho uhai wetu utazidi kuwa mashakani kwa janga la ajali. Poleni sana wafiwa poleni Watanzania kwa ujumla. Njia mwafaka ya kuomboleza msiba huu mkubwa ni kwa kuwakumbuka marehemu katika dua/sala zetu RAIA MWEMA
Makala Yangu RAIA MWEMA La 03/05/17: Uchambuzi Kuhusu JPM Kutimua Wafanyakazi Takriban 10000  MAKALA yangu wiki hii inahusu maoni yangu kuhusu hatua ya serikali ya Rais John Magufuli kufukuza watumishi wa umma takriban 10000 kwa tuhuma za kugushi sifa zao kielimu/ujuzi. Kwanza nitanabaishe mapema kuwa sisi ambao tumetumia sehemu kubwa ya uhai wetu kusaka elimu na tunaendelea kuisaka hatua yoyote dhidi ya wahalifu wa kielimu inastahili pongezi. Kwa hiyo hatua ya serikali dhidi ya watumishi wake walioghushi vyeti/ujuzi ni ya kupongezwa. Haipendezi kuona wadogo zetu wanahitimu kihalali katika ngazi mbalimbali lakini wanakosa ajira kwa vile baadhi ya nafasi za kazi zimekaliwa na watu walioghushi vyeti. Hata hivyo licha ya hatua hiyo inayostahili pongezi kuna kasoro kadhaa. Kwanza kama ilivyokuwa kwa wanafunzi kadhaa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao sio tu walikatishwa masomo yao lakini pia waliiitwa "vilaza" kwa kosa lisilo lao la kuingizwa katika kozi ya ualimu japo alama za ufaulu za baadhi yao zilikuwa za chini. Lengo la serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete kuwachukua wanafunzi hao lilikuwa zuri kwa maana ya mkakati wa kukabiliana na uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi lakini pia kutoa fursa ya pili kwa wanafunzi hao baada ya matokeo yao kutowaruhusu kuendelea na masomo ya kidato cha tano Kama ambavyo wanafunzi hao hawakujichagua wenyewe ndivyo ilivyokuwa kwa watumishi wa umma waliofukuzwa kwa kufoji vyeti. Hawakujiajiri wenyewe. Waliajiriwa. Tumepasua jipu kwa kuwafukuza kazi lakini hatujashughulikia kiini cha jipu hilo. Na kwa kiasi kikubwa kiini ni wanasiasa ambao kama mzaha vile hawakuguswa na zoezi la uhakiki wa vyeti vyao/elimu zao. Uzoefu wangu katika utumishi wa serikali unaonyesha kuwa kwa kiasi kikubwa ajira serikalini zimekuwa zikitolewa sio kwa kuzingatia elimu au uzoefu bali kujuana. Nimeandika kuhusu hilo katika kitabu changu cha #Shushushu (kinachozungumzia kuhusu taaluma ya uafisa usalama wa taifa) kuwa moja ya changamoto kubwa kwa Idara yetu ya Usalama wa Taifa ni mfumo mbovu wa ajira unaotoa fursa ya ajira za kujuana/kubebana. Utumishi katika taasisi kama hiyo unahitaji utiifu kwa taifa lakini ukiajiri mtu kwa vile ni mtoto wa fulani sio tu anakuwa na utiifu zaidi kwa huyo "fulani" kuliko taifa bali pia kunakuwa na dharau ya "ah watanifanya nini wakati fulani aliyeniingiza kazini yupo?" Sasa tumeanza kuwafahamu kwa majina baadhi ya watumishi hao waliofukuzwa kazi. Hata hivyo ni mapema mno kufahamu iwapo hatua hiyo iliwahusu watumishi wote wa umma au wale tu "wasio ndugu jamaa au marafiki wa akina fulani"? Je wale watoto wa vigogo pale Benki Kuu nao waliguswa na zoezi hilo? Je ndugu jamaa na marafiki wa watawala wetu waliojazana kwenye balozi zetu za nje nao waliguswa? "Kitengo" je? Ila jambo moja ninalohisi linaweza kuwa "matokeo yasiyotarajiwa" (unintended consequences) ni uwezekano wa baadhi ya waliofukuzwa kazi kufungua kesi dhidi ya serikali. Kuna kasoro kadhaa za kisheria katika utekelezaji wa amri hiyo ya rais lakini hapa sio mahala pake kuyajadili. Japo siwezi kubashiri matokeo ya kesi hiyo iwapo itafunguliwa vitu viwili vinavyoweza kuongeza uzito wa hoja za watumishi hao ni pamoja na kauli ya Rais Magufuli kwamba "wafungwe miaka saba." Ni kazi ya mahakama kutoa hukumu sio Rais. Na kwa Rais katamka hivyo ni kama anaiamuru mahakama itekeleze matakwa yake badala ya kufuata sheria. Pili ni wazi kuwa serikali imefanya ubaguzi kwa kuendesha zoezi hili kwa kuangalia watumishi wasio vigogo huku ikifumbia macho viongozi mbalimbali ambao baadhi yao wanaendelea kuandamwa na tuhuma sio za kughushi vyeti vya elimu tu bali hata majina (ni nani asiyejua kuhusu suala la Bashite?) Yayumkinika kuituhumu serikali kuwa imekwepa kwa makusudi kuhakiki sio elimu tu bali hata uraia wa viongozi wa kisiasa. Tuna wanasiasa wengi tu wenye elimu au uraia tata. Kwa hiyo japo hatua ya kuhakiki elimu ya watumishi wa umma inastahili pongezi ubaguzi wa makusudi uliofanyika katika zoezi hilo unapaswa kulaaniwa vikali. Lengo halikuwa kumnusuru Bashite pekee bali pia baadhi ya wabunge Wakuu wa mikoa wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa kisiasa ambao baadhi yao sio tu wana walakini kielimu bali pia uraia wao ni tete. FacebookTwitterGoogleWhatsAppPinterestShare  RAIA MWEMA Unintended Consequences, Zuri
Makala Yangu RAIA MWEMA La 03/05/17: Uchambuzi Kuhusu JPM Kutimua Wafanyakazi Takriban 10,000
Makala Yangu RAIA MWEMA La 03/05/17: Uchambuzi Kuhusu JPM Kutimua Wafanyakazi Takriban 10000 MAKALA yangu wiki hii inahusu maoni yangu kuhusu hatua ya serikali ya Rais John Magufuli kufukuza watumishi wa umma takriban 10000 kwa tuhuma za kugushi sifa zao kielimu/ujuzi. Kwanza nitanabaishe mapema kuwa sisi ambao tumetumia sehemu kubwa ya uhai wetu kusaka elimu na tunaendelea kuisaka hatua yoyote dhidi ya wahalifu wa kielimu inastahili pongezi. Kwa hiyo hatua ya serikali dhidi ya watumishi wake walioghushi vyeti/ujuzi ni ya kupongezwa. Haipendezi kuona wadogo zetu wanahitimu kihalali katika ngazi mbalimbali lakini wanakosa ajira kwa vile baadhi ya nafasi za kazi zimekaliwa na watu walioghushi vyeti. Hata hivyo licha ya hatua hiyo inayostahili pongezi kuna kasoro kadhaa. Kwanza kama ilivyokuwa kwa wanafunzi kadhaa wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao sio tu walikatishwa masomo yao lakini pia waliiitwa "vilaza" kwa kosa lisilo lao la kuingizwa katika kozi ya ualimu japo alama za ufaulu za baadhi yao zilikuwa za chini. Lengo la serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete kuwachukua wanafunzi hao lilikuwa zuri kwa maana ya mkakati wa kukabiliana na uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi lakini pia kutoa fursa ya pili kwa wanafunzi hao baada ya matokeo yao kutowaruhusu kuendelea na masomo ya kidato cha tano Kama ambavyo wanafunzi hao hawakujichagua wenyewe ndivyo ilivyokuwa kwa watumishi wa umma waliofukuzwa kwa kufoji vyeti. Hawakujiajiri wenyewe. Waliajiriwa. Tumepasua jipu kwa kuwafukuza kazi lakini hatujashughulikia kiini cha jipu hilo. Na kwa kiasi kikubwa kiini ni wanasiasa ambao kama mzaha vile hawakuguswa na zoezi la uhakiki wa vyeti vyao/elimu zao. Uzoefu wangu katika utumishi wa serikali unaonyesha kuwa kwa kiasi kikubwa ajira serikalini zimekuwa zikitolewa sio kwa kuzingatia elimu au uzoefu bali kujuana. Nimeandika kuhusu hilo katika kitabu changu cha #Shushushu (kinachozungumzia kuhusu taaluma ya uafisa usalama wa taifa) kuwa moja ya changamoto kubwa kwa Idara yetu ya Usalama wa Taifa ni mfumo mbovu wa ajira unaotoa fursa ya ajira za kujuana/kubebana. Utumishi katika taasisi kama hiyo unahitaji utiifu kwa taifa lakini ukiajiri mtu kwa vile ni mtoto wa fulani sio tu anakuwa na utiifu zaidi kwa huyo "fulani" kuliko taifa bali pia kunakuwa na dharau ya "ah watanifanya nini wakati fulani aliyeniingiza kazini yupo?" Sasa tumeanza kuwafahamu kwa majina baadhi ya watumishi hao waliofukuzwa kazi. Hata hivyo ni mapema mno kufahamu iwapo hatua hiyo iliwahusu watumishi wote wa umma au wale tu "wasio ndugu jamaa au marafiki wa akina fulani"? Je wale watoto wa vigogo pale Benki Kuu nao waliguswa na zoezi hilo? Je ndugu jamaa na marafiki wa watawala wetu waliojazana kwenye balozi zetu za nje nao waliguswa? "Kitengo" je? Ila jambo moja ninalohisi linaweza kuwa "matokeo yasiyotarajiwa" (unintended consequences) ni uwezekano wa baadhi ya waliofukuzwa kazi kufungua kesi dhidi ya serikali. Kuna kasoro kadhaa za kisheria katika utekelezaji wa amri hiyo ya rais lakini hapa sio mahala pake kuyajadili. Japo siwezi kubashiri matokeo ya kesi hiyo iwapo itafunguliwa vitu viwili vinavyoweza kuongeza uzito wa hoja za watumishi hao ni pamoja na kauli ya Rais Magufuli kwamba "wafungwe miaka saba." Ni kazi ya mahakama kutoa hukumu sio Rais. Na kwa Rais katamka hivyo ni kama anaiamuru mahakama itekeleze matakwa yake badala ya kufuata sheria. Pili ni wazi kuwa serikali imefanya ubaguzi kwa kuendesha zoezi hili kwa kuangalia watumishi wasio vigogo huku ikifumbia macho viongozi mbalimbali ambao baadhi yao wanaendelea kuandamwa na tuhuma sio za kughushi vyeti vya elimu tu bali hata majina (ni nani asiyejua kuhusu suala la Bashite?) Yayumkinika kuituhumu serikali kuwa imekwepa kwa makusudi kuhakiki sio elimu tu bali hata uraia wa viongozi wa kisiasa. Tuna wanasiasa wengi tu wenye elimu au uraia tata. Kwa hiyo japo hatua ya kuhakiki elimu ya watumishi wa umma inastahili pongezi ubaguzi wa makusudi uliofanyika katika zoezi hilo unapaswa kulaaniwa vikali. Lengo halikuwa kumnusuru Bashite pekee bali pia baadhi ya wabunge Wakuu wa mikoa wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa kisiasa ambao baadhi yao sio tu wana walakini kielimu bali pia uraia wao ni tete. FacebookTwitterGoogleWhatsAppPinterestShare RAIA MWEMA
Makala Yangu RAIA MWEMA La 20/04/17: "Magufuli Ameshiwa Pumzi Ya Kutumbua Majipu?"  NIANZE makala hii kwa kutoa salamu za rambirambi kwa familia za askari wanane wa Jeshi la Polisi waliouawa kinyama wiki iliyopita wilayani Kibiti mkoani Pwani. Huu ni msiba wa kitaifa japo hakuna maombolezo ya kitaifa sijui kwa vile hatuthamini uhai wa Watanzania wenzetu au tumekwishazoea sana vifo kama vile vya ajali. Katika moja ya vitu nilivyojifunza katika miaka yangu kadhaa ya kuishi hapa Uingereza ni jinsi wenzetu wanavyothamini uhai. Laiti tukio hili la kuuawa polisi wanane huko Kibiti ndio lingekuwa limetokea hapa basi huenda kila kitu kingesimama. Na si hapa Uingereza pekee. Kwa hali ilivyo sasa katika baadhi ya mataifa ya Ulaya Magharibi sasa ni kama "tumekwishaanza kuzoea matukio ya kigaidi maana yanatuandama mno hasa Ufaransa Ubelgiji na Ujerumani na majuzi hapa Uingereza. Katika kila tukio bila kujali idadi ya waathirika takriban ndani ya saa moja tangu kutokea tukio husika Rais au Waziri Mkuu wa nchi husika huongea na wananchi katika runinga mubashara kutoa pole kwa waathirika kuwahakikishia usalama wananchi na kuwaonya wahusika kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Huu ndio uongozi. Je sisi hali ikoje? Sana sana ni taarifa ya salamu za rambirambi kutoka kwa Rais matamko ya hapa na pale ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na kauli za vitisho za IGP Ernest Mangu sio kwa majambazi bali wananchi wanaochekelea vifo vya polisi hao waliouawa. Japo sio busara kwa mtu yeyote kufurahia kifo cha mtu mwingine hata kama sio polisi lakini hilo sio kosa la jinai. Kadhalika ni vema nguvu ikaelekezwa kwenye tatizo halisi ambalo Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa IGP Mangu haliwezi kukwepa lawama kwa sababu tishio la usalama mkoani Pwani limedumu kitambo sasa bila kupatiwa ufumbuzi kuliko tatizo la kufikirika (kuwa kuna watu wanafurahia vifo vya polisi hao) Saa kadhaa baada ya kupatikana taarifa za mauaji hayo Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Nsato Marijani alizungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine alinukuliwa akisema kuwa jeshi hilo "halitokuwa na mzaha wala msamaha" katika operesheni maalumu kuhusiana na tukio hilo. Je kulikuwa na mzaha na msamaha kabla ya tukio hilo ambao sasa hautakuwepo wakati wa operesheni husika? Tukiweka kando kasoro hizo jambo moja lililonigusa mno ni kukosekana kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwenye tukio la kuaga miili ya polisi hao. Badala ya kujumuika na wafiwa Rais alihudhuria hafla mbili (ambazo zingeweza kabisa kusogezwa mbele) za uzinduzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na makazi katika kitongoji cha Magomeni. Sambamba na hilo tukilinganisha na matukio makubwa mawili ya hivi karibuni uvamizi uliofanywa na RC Makonda kwenye kituo cha Clouds na "kutekwa" kwa msanii wa bongofleva Roma Mkatoliki mauaji hayo ya polisi hao wanane yalipewa uzito mdogo na Watanzania wengi angalau huko mtandaoni. Hali hiyo inasikitisha lakini haishangazi. Sababu moja kuu ya "wananchi wengi kutoonekana kuguswa na mauaji hayo ya polisi wanane" ni ukweli kwamba uhusiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wengi sio mzuri. Polisi wetu kwa kiasi Fulani wamekuwa wakisifika kwa unyanyasaji dhidi ya raia wasio na hatia. Na kama kuna kitengo cha polisi wetu "kinachochukiwa mno" ni hicho cha FFU (Kikosi cha Kuzuia Ghasia) ambacho askari hao wanane walikuwamo. Japo siungi mkono"chuki" hiyo lakini naelewa jinsi gani Watanzania wengi wasivyopendezwa na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi. Kwa upande mwingine jeshi hilo limekuwa likionekana kama "adui wa kudumu" dhidi ya vyama vya upinzani huku likifanya upendeleo wa wazi kwa chama tawala CCM. Kwa hiyo wakati tunaomboleza vifo hivyo vya polisi hao wanane ni muhimu mno kwa wahusika kuchukua hatua za makusudi kuondoa "uhusiano wa chuki na shaka" uliopo kati ya Jeshi la Polisi na asilimia kubwa ya Watanzania. Kana kwamba uhusiano bora kati ya Jeshi la Polisi na wananchi sio muhimu sana moja ya nyenzo muhimu ya kujenga na kuimarisha ushirikiano huo mpango wa Polisi Jamii ulifutwa kwa sababu wanazozijua wahusika. Polisi jamii ilikuwa kiungo muhimu kati ya polisi wetu na jamii. Kioperesheni japo tukio hilo la mauaji ya polisi wanane linaelezwa kuwa ni la kijambazi binafsi ninahisi kuwa kuna tatizo zaidi ya ujambazi. Na kwa tafsiri ninayoelewa kuhusu ugaidi basi tukio hilo linastahili kabisa kuitwa la kigaidi. Ni majambazi gani wenye ujasiri wa kuwavizia polisi na kuwaua kwa namna hiyo ya uvamizi wa kushitukiza? Halafu hilo sio tukio la kwanza. Na hao polisi wanane sio polisi wa kwanza kuuawa katika eneo hilo sambamba na wakazi wengine. Yayumkinika kuhitimisha kuwa Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani hawawezi kukwepa lawama kwa kushindwa kukabili kushamiri kwa mauaji katika eneo hilo. Sijui Rais Magufuli ameishiwa na zile sindano zake za kutumbulia majipu au kaishiwa pumzi ya TumbuaMajipu lakini ni wazi kuna matatizo ya msingi katika uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kwa ujumla. Ukimya wa polisi katika uvamizi huko Clouds na "kutekwa" kwa Roma na sasa hili la Kibiti vilipaswa kumfanya Rais Magufuli achukue hatua. Moja ya sababu maarufu ya polisi wetu wanapozuia mikutano au maandamano ya vyama vya upinzani huwa "intelijensia." Sasa kama intelijensia ipo kwenye kudhibiti shughuli halali za vyama vya siasa kwa nini intelijensia hiyo isitumike kwenye kukabiliana na "magaidi" hao wanaotikisa Mkoa wa Pwani? Nihitimishe makala hii kwa kurejea salamu zangu za rambirambi kwa familia za askari hao waliouawa kinyama. Pamoja na upungufu wote nilioutanabaisha katika makala hii hakuna kitu chochote kinachoweza kuhalalisha unyama waliofanyiwa askari hao. Lakini pia wakati tunaomboleza vifo vyao ni vema tukatafakari kama taifa kuhusu uhusiano kati ya Jeshi la Polisi (na vyombo vyote vya dola kwa ujumla) na raia ambao ukiwa bora unaweza kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na taifa kwa ujumla RAIA MWEMA Mangu, Vile, Single Breasted Suit Jacket, Rome
Makala Yangu RAIA MWEMA La 20/04/17: "Magufuli Ameshiwa Pumzi Ya Kutumbua Majipu?"
Makala Yangu RAIA MWEMA La 20/04/17: "Magufuli Ameshiwa Pumzi Ya Kutumbua Majipu?" NIANZE makala hii kwa kutoa salamu za rambirambi kwa familia za askari wanane wa Jeshi la Polisi waliouawa kinyama wiki iliyopita wilayani Kibiti mkoani Pwani. Huu ni msiba wa kitaifa japo hakuna maombolezo ya kitaifa sijui kwa vile hatuthamini uhai wa Watanzania wenzetu au tumekwishazoea sana vifo kama vile vya ajali. Katika moja ya vitu nilivyojifunza katika miaka yangu kadhaa ya kuishi hapa Uingereza ni jinsi wenzetu wanavyothamini uhai. Laiti tukio hili la kuuawa polisi wanane huko Kibiti ndio lingekuwa limetokea hapa basi huenda kila kitu kingesimama. Na si hapa Uingereza pekee. Kwa hali ilivyo sasa katika baadhi ya mataifa ya Ulaya Magharibi sasa ni kama "tumekwishaanza kuzoea matukio ya kigaidi maana yanatuandama mno hasa Ufaransa Ubelgiji na Ujerumani na majuzi hapa Uingereza. Katika kila tukio bila kujali idadi ya waathirika takriban ndani ya saa moja tangu kutokea tukio husika Rais au Waziri Mkuu wa nchi husika huongea na wananchi katika runinga mubashara kutoa pole kwa waathirika kuwahakikishia usalama wananchi na kuwaonya wahusika kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Huu ndio uongozi. Je sisi hali ikoje? Sana sana ni taarifa ya salamu za rambirambi kutoka kwa Rais matamko ya hapa na pale ya Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na kauli za vitisho za IGP Ernest Mangu sio kwa majambazi bali wananchi wanaochekelea vifo vya polisi hao waliouawa. Japo sio busara kwa mtu yeyote kufurahia kifo cha mtu mwingine hata kama sio polisi lakini hilo sio kosa la jinai. Kadhalika ni vema nguvu ikaelekezwa kwenye tatizo halisi ambalo Jeshi la Polisi chini ya uongozi wa IGP Mangu haliwezi kukwepa lawama kwa sababu tishio la usalama mkoani Pwani limedumu kitambo sasa bila kupatiwa ufumbuzi kuliko tatizo la kufikirika (kuwa kuna watu wanafurahia vifo vya polisi hao) Saa kadhaa baada ya kupatikana taarifa za mauaji hayo Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Nsato Marijani alizungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine alinukuliwa akisema kuwa jeshi hilo "halitokuwa na mzaha wala msamaha" katika operesheni maalumu kuhusiana na tukio hilo. Je kulikuwa na mzaha na msamaha kabla ya tukio hilo ambao sasa hautakuwepo wakati wa operesheni husika? Tukiweka kando kasoro hizo jambo moja lililonigusa mno ni kukosekana kwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwenye tukio la kuaga miili ya polisi hao. Badala ya kujumuika na wafiwa Rais alihudhuria hafla mbili (ambazo zingeweza kabisa kusogezwa mbele) za uzinduzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na makazi katika kitongoji cha Magomeni. Sambamba na hilo tukilinganisha na matukio makubwa mawili ya hivi karibuni uvamizi uliofanywa na RC Makonda kwenye kituo cha Clouds na "kutekwa" kwa msanii wa bongofleva Roma Mkatoliki mauaji hayo ya polisi hao wanane yalipewa uzito mdogo na Watanzania wengi angalau huko mtandaoni. Hali hiyo inasikitisha lakini haishangazi. Sababu moja kuu ya "wananchi wengi kutoonekana kuguswa na mauaji hayo ya polisi wanane" ni ukweli kwamba uhusiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi wengi sio mzuri. Polisi wetu kwa kiasi Fulani wamekuwa wakisifika kwa unyanyasaji dhidi ya raia wasio na hatia. Na kama kuna kitengo cha polisi wetu "kinachochukiwa mno" ni hicho cha FFU (Kikosi cha Kuzuia Ghasia) ambacho askari hao wanane walikuwamo. Japo siungi mkono"chuki" hiyo lakini naelewa jinsi gani Watanzania wengi wasivyopendezwa na utendaji kazi wa Jeshi la Polisi. Kwa upande mwingine jeshi hilo limekuwa likionekana kama "adui wa kudumu" dhidi ya vyama vya upinzani huku likifanya upendeleo wa wazi kwa chama tawala CCM. Kwa hiyo wakati tunaomboleza vifo hivyo vya polisi hao wanane ni muhimu mno kwa wahusika kuchukua hatua za makusudi kuondoa "uhusiano wa chuki na shaka" uliopo kati ya Jeshi la Polisi na asilimia kubwa ya Watanzania. Kana kwamba uhusiano bora kati ya Jeshi la Polisi na wananchi sio muhimu sana moja ya nyenzo muhimu ya kujenga na kuimarisha ushirikiano huo mpango wa Polisi Jamii ulifutwa kwa sababu wanazozijua wahusika. Polisi jamii ilikuwa kiungo muhimu kati ya polisi wetu na jamii. Kioperesheni japo tukio hilo la mauaji ya polisi wanane linaelezwa kuwa ni la kijambazi binafsi ninahisi kuwa kuna tatizo zaidi ya ujambazi. Na kwa tafsiri ninayoelewa kuhusu ugaidi basi tukio hilo linastahili kabisa kuitwa la kigaidi. Ni majambazi gani wenye ujasiri wa kuwavizia polisi na kuwaua kwa namna hiyo ya uvamizi wa kushitukiza? Halafu hilo sio tukio la kwanza. Na hao polisi wanane sio polisi wa kwanza kuuawa katika eneo hilo sambamba na wakazi wengine. Yayumkinika kuhitimisha kuwa Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani hawawezi kukwepa lawama kwa kushindwa kukabili kushamiri kwa mauaji katika eneo hilo. Sijui Rais Magufuli ameishiwa na zile sindano zake za kutumbulia majipu au kaishiwa pumzi ya TumbuaMajipu lakini ni wazi kuna matatizo ya msingi katika uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kwa ujumla. Ukimya wa polisi katika uvamizi huko Clouds na "kutekwa" kwa Roma na sasa hili la Kibiti vilipaswa kumfanya Rais Magufuli achukue hatua. Moja ya sababu maarufu ya polisi wetu wanapozuia mikutano au maandamano ya vyama vya upinzani huwa "intelijensia." Sasa kama intelijensia ipo kwenye kudhibiti shughuli halali za vyama vya siasa kwa nini intelijensia hiyo isitumike kwenye kukabiliana na "magaidi" hao wanaotikisa Mkoa wa Pwani? Nihitimishe makala hii kwa kurejea salamu zangu za rambirambi kwa familia za askari hao waliouawa kinyama. Pamoja na upungufu wote nilioutanabaisha katika makala hii hakuna kitu chochote kinachoweza kuhalalisha unyama waliofanyiwa askari hao. Lakini pia wakati tunaomboleza vifo vyao ni vema tukatafakari kama taifa kuhusu uhusiano kati ya Jeshi la Polisi (na vyombo vyote vya dola kwa ujumla) na raia ambao ukiwa bora unaweza kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na taifa kwa ujumla RAIA MWEMA
Mauaji Ya Polisi Wanane: Maombolezo Maswali Magumu na Ukweli Mchungu  Nianze makala hii kwa kutoa salamu za rambirambi kwa familia za askari wanane wa Jeshi letu la Polisi waliouawa kinyama wilayani Kibiti Mkoani Pwani. Huu ni msiba wa kitaifa japo hakuna maombolezo ya kitaifa - sijui kwa vile hatuthamini uhai wa Watanzania wenzetu au tushazowea sana vifo kama vile vya ajali nk. Jambo moja lililonikera mno jana ni ukimya wa wahusika na mpaka wakati ninaandika makala hii sijasikia kauli yoyote kutoka kwa Inspekta Jenerali wa Polisi. Labda kuna watakaosema "aanasubiri taarifa kamili." Hapana. Uongozi hauko hivyo. Sie huku Ulaya sasa ni kama "tumeshaanza kuzowea" matukio ya kigaidi maana yanatuandama mno hasa Ufaransa Ubelgiji na Ujerumani na majuzi hapa Uingereza. Katika kila tukio bila kujali idadi ya waathirika takriban ndani ya saa moja tangu kutokea tukio husika Rais au Waziri Mkuu wa nchi husika huongea na wananchi katika runinga mubashara kutoa pole kwa waathirika kuwahakikishia usalama wananchi na kuwaonya wahusika kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Huu ndio uongozi. Je sie hali ikoje? Sana sana ni taarifa ya salamu za rambirambi kutoka kwa Rais kama inavyoonekana hapa chini Hadi wakati salamu hizo za rambirambi zinatolewa hakukuwa na tamko lolote kutoka kwa uongozi wa jeshi la polisi. Awali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alithibitisha kutokea kwa tukio hilolakina akadai "hana taarifa" kuhusu tukio hilo hadi atakapowasiliana na IGP. Askari WANANE wameuawa no word from Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi... na "wengineo" waliostahili kuwa wa kwanza kutoa tamko! #Majipu http://pic.twitter.com/bBF0ecBxTU  Evarist Chahali (@Chahali) April 14 2017 Baadaye Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Nsato Marijani aliongea na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine alinukuliwa akisema kuwa jeshi hilo "halitokuwa na mzaha wala msamaha" katika operesheni maalum kuhusiana na tukio hilo 'Kuanzia sasa jeshi la polisi linakwenda kwenye oparesheni maalumu hatutokuwa na mzaha wala msamaha'-Nsato Marijani http://pic.twitter.com/Naytv9A5do  millard ayo (@millardayo) April 14 2017 Je kulikuwa na mzaha na msamaha kabla ya tukio hilo ambao sasa hautokuwepo wakati wa operesheni husika? Tukiweka kando kasoro hizo jambo moja lililonigusa mno ni ukweli kwamba matukio makubwa mawili ya hivi karibuni - uvamizi uliofanywa na RC Makonda kwenye kituo cha Clouds na "kutekwa" kwa msanii wa bongofleva Roma Mkatoliki - yalipewa uzito mkubwa na Watanzania kuliko mauaji hayo ya polisi hao wanane. Inasikitisha lakini haishangazi. Sababu moja kuu ya "wananchi wengi kutoonekana kuguswa na mauaji hayo ya polisi wanane" ni ukweli kwamba mahusiano katika ya Jeshi la Polisi na wananchi wengi sio mazuri. Polisi wetu wamekuwa wakisifika kwa unyanyasaji dhidi ya raia wasio na hatia. Na kama kuna kitengo cha Polisi wetu "kinachochukiwa mno" ni hicho cha FFU (Kikosi cha Kuzuwia Ghasia) ambacho askari hao wanane walikuwamo. Japo siungo "chuki" hiyo lakini naelewa jinsi gani Watanzania wengi wasivyopendezwa na utendaji kazi wa jeshi la polisi. Kwa upande mwingine Jeshi hilo limekuwa likionekana kama "adui wa kudumu" dhidi ya vyama vya upinzani huku likifanya upendeleo wa wazi kwa chama tawala CCM. Kwahiyo wakati tunaomboleza vifo hivyo vya polisi hao wanane ni muhimu mno kwa wahusika kuchukua hatua za makusudi kuondoa "uhusiano wa chuki na mashaka" uliopo kati ya jeshi la polisi na asilimia kubwa ya Watanzania. Kana kwamba uhusiano bora kati ya jeshi la polisi na wananchi sio muhimu "kihivyo" moja ya nyenzo muhimu ya kujenga na kuimarisha ushirikiano huo mpango wa 'Polisi Jamii' ulifutwa kwa sababu wanazozijua wahusika. Polisi jamii ilikuwa kiungo muhimu kati ya polisi wetu na jamii. Kioperesheni japo tukio hilo la mauaji ya polisi wanane linaelezwa kuwa ni la kijambazi binafsi ninahisi kuwa kuna tatizo zaidi ya ujambazi. Na kwa tafsiri ninayoelewa kuhusu ugaidi basi tukio hilo linastahili kabisa kuitwa la kigaidi. Ni majambazi gani wenye ujasiri wa kuwavizia polisi na kuwaua kufuatia 'ambush' kama hiyo iliyotokea eneo la tukio? Halafu hilo sio tukio la kwanza. Na hao polisi wanane sio polisi wa kwanza kuuawa katika eneo hilo sambamba na wakazi wengine. Yayumkinika kuhitimisha kuwa jeshi la polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani hawawezi kukwepa lawama kwa kushindwa kukabili kushamiri kwa mauaji katika eneo hilo. Sijui Rais Magufuli ameishiwa na zile sindano zake za kutumbulia majipu au kaishiwa pumzi ya #TumbuaMajipu lakini ni wazi kuna matatizo ya msingi katika uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na jeshi la polisi kwa ujumla. Ukimya wa polisi katika uvamizi huko Clouds na "kutekwa" kwa Roma na sasa hili la Kibiti vilipaswa kumfanya Rais Magufuli achukue hatua. Moja ya sababu maarufu ya polisi wetu wanapozuwia mikutano au maandamani ya vyama vya upinzani huwa "intelijensia." Sasa kama intelijensia ipo kwenye kudhibiti shughuli halali za vyama vya siasa kwanini intelijensia hiyo isitumike kwenye kukabiliana na "magaidi" hao wanaotikisa Mkoa wa Pwani? Nihitimishe makala hii kwa kurejea salamu zangu za rambirambi kwa familia za askari hao waliouawa kinyama. Pamoja na mapungufu yote niliyotanabaisha katika makala hii hakuna kitu chochote kinachoweza kuhalalisha unyama waliofanyiwa askari hao. Lakini pia wakati tunaomboleza vifo vyao ni vema tukatafakari kama Taifa kuhusu mahusiano kati ya jeshi la polisi (na vyombo vyote vya dola kwa ujumla) na raia ambayo yakiwa bora yanaweza kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na taifa kwa ujumla JESHI LA POLISI TANZANIA Chini, Monster Trucks
Mauaji Ya Polisi Wanane: Maombolezo, Maswali Magumu na Ukweli Mchungu
Mauaji Ya Polisi Wanane: Maombolezo Maswali Magumu na Ukweli Mchungu Nianze makala hii kwa kutoa salamu za rambirambi kwa familia za askari wanane wa Jeshi letu la Polisi waliouawa kinyama wilayani Kibiti Mkoani Pwani. Huu ni msiba wa kitaifa japo hakuna maombolezo ya kitaifa - sijui kwa vile hatuthamini uhai wa Watanzania wenzetu au tushazowea sana vifo kama vile vya ajali nk. Jambo moja lililonikera mno jana ni ukimya wa wahusika na mpaka wakati ninaandika makala hii sijasikia kauli yoyote kutoka kwa Inspekta Jenerali wa Polisi. Labda kuna watakaosema "aanasubiri taarifa kamili." Hapana. Uongozi hauko hivyo. Sie huku Ulaya sasa ni kama "tumeshaanza kuzowea" matukio ya kigaidi maana yanatuandama mno hasa Ufaransa Ubelgiji na Ujerumani na majuzi hapa Uingereza. Katika kila tukio bila kujali idadi ya waathirika takriban ndani ya saa moja tangu kutokea tukio husika Rais au Waziri Mkuu wa nchi husika huongea na wananchi katika runinga mubashara kutoa pole kwa waathirika kuwahakikishia usalama wananchi na kuwaonya wahusika kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Huu ndio uongozi. Je sie hali ikoje? Sana sana ni taarifa ya salamu za rambirambi kutoka kwa Rais kama inavyoonekana hapa chini Hadi wakati salamu hizo za rambirambi zinatolewa hakukuwa na tamko lolote kutoka kwa uongozi wa jeshi la polisi. Awali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alithibitisha kutokea kwa tukio hilolakina akadai "hana taarifa" kuhusu tukio hilo hadi atakapowasiliana na IGP. Askari WANANE wameuawa no word from Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi... na "wengineo" waliostahili kuwa wa kwanza kutoa tamko! #Majipu http://pic.twitter.com/bBF0ecBxTU Evarist Chahali (@Chahali) April 14 2017 Baadaye Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Nsato Marijani aliongea na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine alinukuliwa akisema kuwa jeshi hilo "halitokuwa na mzaha wala msamaha" katika operesheni maalum kuhusiana na tukio hilo 'Kuanzia sasa jeshi la polisi linakwenda kwenye oparesheni maalumu hatutokuwa na mzaha wala msamaha'-Nsato Marijani http://pic.twitter.com/Naytv9A5do millard ayo (@millardayo) April 14 2017 Je kulikuwa na mzaha na msamaha kabla ya tukio hilo ambao sasa hautokuwepo wakati wa operesheni husika? Tukiweka kando kasoro hizo jambo moja lililonigusa mno ni ukweli kwamba matukio makubwa mawili ya hivi karibuni - uvamizi uliofanywa na RC Makonda kwenye kituo cha Clouds na "kutekwa" kwa msanii wa bongofleva Roma Mkatoliki - yalipewa uzito mkubwa na Watanzania kuliko mauaji hayo ya polisi hao wanane. Inasikitisha lakini haishangazi. Sababu moja kuu ya "wananchi wengi kutoonekana kuguswa na mauaji hayo ya polisi wanane" ni ukweli kwamba mahusiano katika ya Jeshi la Polisi na wananchi wengi sio mazuri. Polisi wetu wamekuwa wakisifika kwa unyanyasaji dhidi ya raia wasio na hatia. Na kama kuna kitengo cha Polisi wetu "kinachochukiwa mno" ni hicho cha FFU (Kikosi cha Kuzuwia Ghasia) ambacho askari hao wanane walikuwamo. Japo siungo "chuki" hiyo lakini naelewa jinsi gani Watanzania wengi wasivyopendezwa na utendaji kazi wa jeshi la polisi. Kwa upande mwingine Jeshi hilo limekuwa likionekana kama "adui wa kudumu" dhidi ya vyama vya upinzani huku likifanya upendeleo wa wazi kwa chama tawala CCM. Kwahiyo wakati tunaomboleza vifo hivyo vya polisi hao wanane ni muhimu mno kwa wahusika kuchukua hatua za makusudi kuondoa "uhusiano wa chuki na mashaka" uliopo kati ya jeshi la polisi na asilimia kubwa ya Watanzania. Kana kwamba uhusiano bora kati ya jeshi la polisi na wananchi sio muhimu "kihivyo" moja ya nyenzo muhimu ya kujenga na kuimarisha ushirikiano huo mpango wa 'Polisi Jamii' ulifutwa kwa sababu wanazozijua wahusika. Polisi jamii ilikuwa kiungo muhimu kati ya polisi wetu na jamii. Kioperesheni japo tukio hilo la mauaji ya polisi wanane linaelezwa kuwa ni la kijambazi binafsi ninahisi kuwa kuna tatizo zaidi ya ujambazi. Na kwa tafsiri ninayoelewa kuhusu ugaidi basi tukio hilo linastahili kabisa kuitwa la kigaidi. Ni majambazi gani wenye ujasiri wa kuwavizia polisi na kuwaua kufuatia 'ambush' kama hiyo iliyotokea eneo la tukio? Halafu hilo sio tukio la kwanza. Na hao polisi wanane sio polisi wa kwanza kuuawa katika eneo hilo sambamba na wakazi wengine. Yayumkinika kuhitimisha kuwa jeshi la polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani hawawezi kukwepa lawama kwa kushindwa kukabili kushamiri kwa mauaji katika eneo hilo. Sijui Rais Magufuli ameishiwa na zile sindano zake za kutumbulia majipu au kaishiwa pumzi ya #TumbuaMajipu lakini ni wazi kuna matatizo ya msingi katika uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani na jeshi la polisi kwa ujumla. Ukimya wa polisi katika uvamizi huko Clouds na "kutekwa" kwa Roma na sasa hili la Kibiti vilipaswa kumfanya Rais Magufuli achukue hatua. Moja ya sababu maarufu ya polisi wetu wanapozuwia mikutano au maandamani ya vyama vya upinzani huwa "intelijensia." Sasa kama intelijensia ipo kwenye kudhibiti shughuli halali za vyama vya siasa kwanini intelijensia hiyo isitumike kwenye kukabiliana na "magaidi" hao wanaotikisa Mkoa wa Pwani? Nihitimishe makala hii kwa kurejea salamu zangu za rambirambi kwa familia za askari hao waliouawa kinyama. Pamoja na mapungufu yote niliyotanabaisha katika makala hii hakuna kitu chochote kinachoweza kuhalalisha unyama waliofanyiwa askari hao. Lakini pia wakati tunaomboleza vifo vyao ni vema tukatafakari kama Taifa kuhusu mahusiano kati ya jeshi la polisi (na vyombo vyote vya dola kwa ujumla) na raia ambayo yakiwa bora yanaweza kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na taifa kwa ujumla JESHI LA POLISI TANZANIA
Makala Yangu RAIA MWEMA la 12.04.17: Kwa Matukio Haya Hali Ya Utulivu TZ Ipo Mashakani  WANASEMA wiki nzima katika siasa ni sawa na uhai mzima wa mwanadamu. Maana ya msemo huo ni kwamba katika siasa tunaweza kushuhudia matukio mengi katika muda mfupi tu. Kwa lugha nyingine katika siasa hata wiki tu ni ndefu kama uhai mzima. Sasa kama wiki tu ni uhai mzima je hali ikoje kwa mwaka mzima? Pengine jawabu lipo kwenye kuiangalia Tanzania yetu katika kipindi cha takriban mwaka na nusu sasa kutoka zam Swahili, Bbc, Fictional Characters, Fantasy Characters
Makala Yangu RAIA MWEMA la 12.04.17: Kwa Matukio Haya, Hali Ya Utulivu TZ Ipo Mashakani
Makala Yangu RAIA MWEMA la 12.04.17: Kwa Matukio Haya Hali Ya Utulivu TZ Ipo Mashakani WANASEMA wiki nzima katika siasa ni sawa na uhai mzima wa mwanadamu. Maana ya msemo huo ni kwamba katika siasa tunaweza kushuhudia matukio mengi katika muda mfupi tu. Kwa lugha nyingine katika siasa hata wiki tu ni ndefu kama uhai mzima. Sasa kama wiki tu ni uhai mzima je hali ikoje kwa mwaka mzima? Pengine jawabu lipo kwenye kuiangalia Tanzania yetu katika kipindi cha takriban mwaka na nusu sasa kutoka zam
TATHMINI: JPM Kumteua Prof Kitila Ukatibu Mkuu Wa Wizara Na Zitto Kumsapoti JPM  Habari iliyotawala mno jana ni taarifa kutoka Ikulu kuwa Rais John Magufuli amemteua kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo Profesa Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji. Kwa tathmini ya haraka haraka taarifa hiyo imepokelewa kwa mitazamo miwili: wanaounga mkono hatua hiyo na wanaoipinga. Wanaoiunga mkono wanaona hatua hiyo ya Magufuli kama mwafaka katika kujenga umoja wa kitaifa na ushirikiano bila kujali tofauti za kiitikadi. Wanaopinga wanaona uteuzi huo umelenga kuidhoofisha ACT-Wazalendo mtego ambao haijulikani una malengo gani na unafiki wa baadhi ya wanasiasa wa upinzani - katika suala hili ni Profesa Kitila na bosi wake Zitto Kabwe ambaye tayari amepongeza uteuzi huo. Kwa sie tunaoliangalia suala hili 'kwa jicho la tatu' tunabakiwa na maswali mengi yasiyo na majibu. Swali mojawapo ni hili: katika hotuba yake moja huko Zanzibar Rais Magufuli aliapa kutowashirikisha wapinzani kwenye serikali yake (msikilize mwenyewe kwenye video hii hapa chini) Je Prof Kitila alikuwa 'mpinzani feki kwenye chama feki cha upinzani?' Na ukiangalia 'upendeleo' aliopewa Profesa Kitila katika wadhifa wake kama mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kisha ukalinganisha na sababu zilizoplekea Profesa Mwesiga Baregu asiongezewe mkataba chuoni hapo utahisi ipo namna. Hadi wakati Profesa Kitila anapewa 'ulaji' na Magufuli ushiriki wake kwenye siasa haukuwa tatizo kwa serikali hiyohiyo 'iliyomkalia kooni' Profesa mzoefu Barefu. Lakini pengine unafiki mkubwa wa Profesa Kitila ni ukweli kwamba alishaweka msimamo wake huko nyuma alipokemea teuzi zinazofanywa na Rais Magufuli kuwachukua wahadhiri pasipo kuandaa wa kurithi nafasi zao. Hello Prof @kitilam http://pic.twitter.com/bW0qFJjLVr  Evarist Chahali (@Chahali) April 4 2017 Kwahiyo sidhani kama kuna neno stahili kuhusu Profesa Kitila zaidi ya unafiki. Ndio alikuwa mtumishi wa serikali lakini pia alikuwa kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo. Na hili la unafiki linahusu kotekote kwenye kazi yake kama mhadhiri - aliyekwishakemea tabia ya serikali kupora wasomi kwenye taasisi za elimu - na kama mwanasiasa ambaye baadhi yetu tulikuwa tukimwona kama tegemeo japo kiduchu kwenye siasa za upinzani. Leo hii Profesa Kitila ameibuliwa kutoka UDSM na ACT-Wazalendo katika namla ileile BASHITE alivyoibuliwa kwenye u-DC na kupewa u-RC. Kuhusu Zitto mie kitambo nimekuwa nikimwona kama mwanasiasa mnafiki. Nani asiyekumbuka ahadi yake ya kutaja majina ya mafisadi walioficha pesa za umma huko Uswisi? Na ni Zitto huyu huyu aliyewahi kurushiwa tuhuma za kuisaliti Chadema baada ya gazeti moja kudaka kile ilichodai kuwa mawasiliano kati ya mwanasiasa huyo na kiongozi mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa. Unaweza kuisoma stori husika HAPA. Hivi majuzi tu kulikuwa na tetesi kuwa "Zitto amepotea" Baadaye "akapatikana" na "akamwashia moto" Rais Magufuli akidai kuwa atakuwa rais wa muhula mmoja tu. Mwanasiasa huyo machachari alilaani kile alichoita "tabia za kidikteta za Magufuli" na kwamba "Watanzania hawatamvumilia (Magufuli) kuwatawala kwa kuwaburuza kidikteta." Muda si muda kukajiri 'drama nyingine' kuhusu Zitto ambaye inaelezwa kuwa alilazimika kujificha ndani ya jengo la Bunge ili asikamatwe na polisi. Leo Magufuli kamteua Profesa Kitila kuwa katibu mkuu katika moja ya miujiza ya kisiasa nchini Tanzania na tayari Zitto 'amebadilika.' Hebu msikie hapa chini Uzuri mmoja wa unafiki huu ni kwamba Magufuli kawarushia kitanzi Profesa Kitila na Zitto wajifunge wenyewe au wakikwepe. Kwa sababu wanazozijua wenyewe wamejifunga wenyewe. Nasema hivyo kwa sababu kwa sasa haitowezekana kwa Profesa Kitila kuikosoa serikali kutokana na wadhifa wake huo mpya. Kadhalika Zitto na ACT- Wazalendo yake watakuwa na wakati mgumu kuikosoa serikali ambayo "nao wamo" kupitia uwepo wa Prof Kitila. Lakini pengine ni vema kukumbuka historia ya wawili hawa katika siasa za upinzani Tanzania. Mie ni mmoja wa watu wanaoamini kwa dhati kuwa laiti wawili hao - Zitto na Kitila - wasingefanya chokochoko ambazo baadaye zilipelekea kufukuzwa kao huko Chadema basi huenda leo hii Chadema ingekuwa chama tawala. Nimaliie makala hii kwa kutahadharisha kuwa si ajabu katika siku chache zijazo mtamskia tena Zitto huyuhuyu anayemwagia sifa Magufuli akielezea kuhusu ishu moja nzito. Baadhi yetu twafahamu kuhusu mkakati fulani dhalimu unaomhusisha Bashite dhidi ya watu flani. Ninatarajia Zitto ataufahamu hivi karibuni. Tuliache hilo muda utaongea. Nawatakia siku njema Kitila Mkumbo Magufuli ZITTO KABWE Kuna, Wake, Acting
TATHMINI: JPM Kumteua Prof Kitila Ukatibu Mkuu Wa Wizara Na Zitto Kumsapoti JPM
TATHMINI: JPM Kumteua Prof Kitila Ukatibu Mkuu Wa Wizara Na Zitto Kumsapoti JPM Habari iliyotawala mno jana ni taarifa kutoka Ikulu kuwa Rais John Magufuli amemteua kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo Profesa Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji. Kwa tathmini ya haraka haraka taarifa hiyo imepokelewa kwa mitazamo miwili: wanaounga mkono hatua hiyo na wanaoipinga. Wanaoiunga mkono wanaona hatua hiyo ya Magufuli kama mwafaka katika kujenga umoja wa kitaifa na ushirikiano bila kujali tofauti za kiitikadi. Wanaopinga wanaona uteuzi huo umelenga kuidhoofisha ACT-Wazalendo mtego ambao haijulikani una malengo gani na unafiki wa baadhi ya wanasiasa wa upinzani - katika suala hili ni Profesa Kitila na bosi wake Zitto Kabwe ambaye tayari amepongeza uteuzi huo. Kwa sie tunaoliangalia suala hili 'kwa jicho la tatu' tunabakiwa na maswali mengi yasiyo na majibu. Swali mojawapo ni hili: katika hotuba yake moja huko Zanzibar Rais Magufuli aliapa kutowashirikisha wapinzani kwenye serikali yake (msikilize mwenyewe kwenye video hii hapa chini) Je Prof Kitila alikuwa 'mpinzani feki kwenye chama feki cha upinzani?' Na ukiangalia 'upendeleo' aliopewa Profesa Kitila katika wadhifa wake kama mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kisha ukalinganisha na sababu zilizoplekea Profesa Mwesiga Baregu asiongezewe mkataba chuoni hapo utahisi ipo namna. Hadi wakati Profesa Kitila anapewa 'ulaji' na Magufuli ushiriki wake kwenye siasa haukuwa tatizo kwa serikali hiyohiyo 'iliyomkalia kooni' Profesa mzoefu Barefu. Lakini pengine unafiki mkubwa wa Profesa Kitila ni ukweli kwamba alishaweka msimamo wake huko nyuma alipokemea teuzi zinazofanywa na Rais Magufuli kuwachukua wahadhiri pasipo kuandaa wa kurithi nafasi zao. Hello Prof @kitilam http://pic.twitter.com/bW0qFJjLVr Evarist Chahali (@Chahali) April 4 2017 Kwahiyo sidhani kama kuna neno stahili kuhusu Profesa Kitila zaidi ya unafiki. Ndio alikuwa mtumishi wa serikali lakini pia alikuwa kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo. Na hili la unafiki linahusu kotekote kwenye kazi yake kama mhadhiri - aliyekwishakemea tabia ya serikali kupora wasomi kwenye taasisi za elimu - na kama mwanasiasa ambaye baadhi yetu tulikuwa tukimwona kama tegemeo japo kiduchu kwenye siasa za upinzani. Leo hii Profesa Kitila ameibuliwa kutoka UDSM na ACT-Wazalendo katika namla ileile BASHITE alivyoibuliwa kwenye u-DC na kupewa u-RC. Kuhusu Zitto mie kitambo nimekuwa nikimwona kama mwanasiasa mnafiki. Nani asiyekumbuka ahadi yake ya kutaja majina ya mafisadi walioficha pesa za umma huko Uswisi? Na ni Zitto huyu huyu aliyewahi kurushiwa tuhuma za kuisaliti Chadema baada ya gazeti moja kudaka kile ilichodai kuwa mawasiliano kati ya mwanasiasa huyo na kiongozi mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa. Unaweza kuisoma stori husika HAPA. Hivi majuzi tu kulikuwa na tetesi kuwa "Zitto amepotea" Baadaye "akapatikana" na "akamwashia moto" Rais Magufuli akidai kuwa atakuwa rais wa muhula mmoja tu. Mwanasiasa huyo machachari alilaani kile alichoita "tabia za kidikteta za Magufuli" na kwamba "Watanzania hawatamvumilia (Magufuli) kuwatawala kwa kuwaburuza kidikteta." Muda si muda kukajiri 'drama nyingine' kuhusu Zitto ambaye inaelezwa kuwa alilazimika kujificha ndani ya jengo la Bunge ili asikamatwe na polisi. Leo Magufuli kamteua Profesa Kitila kuwa katibu mkuu katika moja ya miujiza ya kisiasa nchini Tanzania na tayari Zitto 'amebadilika.' Hebu msikie hapa chini Uzuri mmoja wa unafiki huu ni kwamba Magufuli kawarushia kitanzi Profesa Kitila na Zitto wajifunge wenyewe au wakikwepe. Kwa sababu wanazozijua wenyewe wamejifunga wenyewe. Nasema hivyo kwa sababu kwa sasa haitowezekana kwa Profesa Kitila kuikosoa serikali kutokana na wadhifa wake huo mpya. Kadhalika Zitto na ACT- Wazalendo yake watakuwa na wakati mgumu kuikosoa serikali ambayo "nao wamo" kupitia uwepo wa Prof Kitila. Lakini pengine ni vema kukumbuka historia ya wawili hawa katika siasa za upinzani Tanzania. Mie ni mmoja wa watu wanaoamini kwa dhati kuwa laiti wawili hao - Zitto na Kitila - wasingefanya chokochoko ambazo baadaye zilipelekea kufukuzwa kao huko Chadema basi huenda leo hii Chadema ingekuwa chama tawala. Nimaliie makala hii kwa kutahadharisha kuwa si ajabu katika siku chache zijazo mtamskia tena Zitto huyuhuyu anayemwagia sifa Magufuli akielezea kuhusu ishu moja nzito. Baadhi yetu twafahamu kuhusu mkakati fulani dhalimu unaomhusisha Bashite dhidi ya watu flani. Ninatarajia Zitto ataufahamu hivi karibuni. Tuliache hilo muda utaongea. Nawatakia siku njema Kitila Mkumbo Magufuli ZITTO KABWE